Ninayo mafupi tu kwa TFF kuhusu timu yetu Pendwa iliyobugizwa magoli lukuki huko misri.
Action plan kwa TFF:
Vunja bechi la ufundi - tukae bila timu kwa muda tujitafakari - kuanza upya si ujinga
Wekeni mjadala wa wazi muongee na wadau wa soka ili kujua nini cha kufanya na tumejikwaa wapi.
Uteuzi wa Mkuu wa bechi la ufundi (Kocha) uwe wa wazi - Tangazeni kazi hiyo kwenye gazeti la Serikali watu waone mchakato mzima unavyokwenda na siyo kutuletea mtu sijui alicheza mpira zamani miaka hiyo ndiyo kiwe kigezo - kama ni mpira hata kina Madata Lubigisa, Kasongo Athuman na kina Tenze mbona walicheza fresh tu.
Kataeni kabisa wanasiasa kuingilia mambo ya timu - hii ni kuwagawa watanzania - kwanza wanawachanganya wachezaji kwa kutoa hadi za ajabu ajabu zile za kunenepesha ngombe siku ya mnada - vijana wanapagawa wanacheza kuwa kuchechemea....waacheni wa -relax na si kiongozi yupo pale mimacho katoa kama pima.
Tafuteni vijana bora under 15 kwenye kila idara uwanjani - ubora uendane na umri, urefu na wajihi - vijana hawa walau 30 tu best watafutieni timu nje ya nchi - Serikali haishindwi jamani - pamoja na kocha mbovu ila na watu wenyewe hawaeleweki - eti benki wa pembeni ana urefu wa nchi 3 ulishaona wapi duniani
Nisiwachoshe ni hayo tu - Vunja timu kuanza upya si ujinga.