TFF kuilipa kampuni ya Romario Sports 2010 Limited Tsh. Milioni 843 za Deni na Fidia

TFF kuilipa kampuni ya Romario Sports 2010 Limited Tsh. Milioni 843 za Deni na Fidia

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limefikia makubaliano nje ya mahakama katika shauri la madai lililokuwa limefunguliwa na kampuni ya Romario Sports 2010 Limited, kwa kuilipa kampuni hiyo deni pamoja na fidia.

Kulingana na hukumu ya makubaliano (consent judgement) iliyotolewa na Jaji Isaya Arufani wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, TFF itailipa kampuni hiyo jumla ya Sh843 Milioni kama deni pamoja na fidia mbalimbali.

Kiini cha mgogoro huo ni hatua ya TFF kutolipa deni la Sh843 milioni lililotokana na kampuni ya Romario Sports 2010 Limited, kuiuzia TFF vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya Sh 893 milioni na hivyo kuingia katika mgogoro.

Baada ya TFF kushindwa kulipa deni hilo, kampuni hiyo iliwasiliana na TFF ili kujaribu kumaliza suala hilo kwa njia ya amani na wakakubaliana na TFF kuwa wangelipa fedha hizo kwa awamu 18 kuanzia Januari 31, 2023 hadi Juni 30,2024.

Hata hivyo, makubaliano hayo ya kumaliza deni hilo kwa njia ya amani hayakuzaa matunda na kusababisha kampuni hiyo kuamua kufungua shauri la madai namba 9792 la 2024 katika mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo, kampuni hiyo ilikuwa inaiomba mahakama itamke kuwa TFF imevunja makubaliano waliyoingia Februari 2,2023, walipe deni lote wanalodaiwa, kulipa fidia ya jumla ya Sh200 milioni na kulipa fidia ya hasara ya Sh300 milioni.

Pia mahakama iamuru TFF kulipa riba ambayo mahakama itaamuru kama fidia ya uharibifu na fidia ya jumla ambayo jumla yake ni Sh500 milioni na riba hiyo italipwa katika viwango vya kibiashara vinavyotozwa na mabenki.

MWANANCHI
 
consent judgement) iliyotolewa na Jaji Isaya Arufani wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, TFF itailipa kampuni hiyo jumla ya Sh1.69 bilioni kama deni pamoja na fidia mbalimbali.
Dawa ya deni ni kulipa, TFF hamna jinsi ya kukwepa
Judgement:
I. That, the defendant shall pay the plaintiff the outstanding amount of TZS. 843,039,240/= hereinafter called the settlement sum.

II. That the defendant shall pay to the plaintiff TZS. 50,000,000/ =
every month starting from the end of August, September to October of 2024 totaling to TZS. 150,000,000/ = .

III. That, the defendant shall pay to plaintiff every month from November of 2024 TZS. 100,000,000/= to May of 2025 totaling TZS. 700,000,000/ = .
IV. That both parties agreed that this Settlement Agreement be adopted as court judgment and decree and executable upon failure of the defendant to pay any of the agreed installments.

V. That, upon the failure of the defendant to pay the plaintiff any monthly installments as agreed in here, the plaintiff shall proceed to execute for the entire amount outstanding as in the settlement.

It is so ordered.
JUDGE
19/08/2024

Read more : Romario Sports 2010 Limited vs Tanzania Football Federation (Civil Case No. 9792 of 2024) [2024] TZHC 7322 (19 August 2024)
 
Huyu mnufaika ambaye hakulipwa miaka yote hii wakurugenzi wake ni kina nani Romario Sports

1724161556187.png

Minhaal Dewji. Managing Director at Romario Sports...
 
Naona ule msemo wa kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake unafanya kazi ipasavyo.
 
Back
Top Bottom