Black Opal
JF-Expert Member
- Jan 22, 2023
- 233
- 298
Mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA hufanyika kwenye ngazi ya shule ya msingi pamoja na sekondari ikijumuisha michezo mbalimbali kama vile soka, netiboli, mpira wa mikono, nk, ambapo mashindano huanzia kwenye ngazi ya chini hadi kufikia ngazi taifa ambapo mwisho hupatikana kikosi cha taifa. Kwa miaka mingi mashindano yakiisha washindi wanapewa zawadi na inaisha hivyo, mwaka mwingine ukifika mambo yanaendelea vile vile. Tunapoteza rasilimali lakini pia tunapoteza vipaji vingi wakati tuna nafasi ya kukuza vijana hawa kuja kuwa wachezaji wakubwa nchini na hata kimataifa.
Nakumbuka nilivyokuwa sekondari tulishiriki kwenye mashindano haya. Shule yetu ilishiriki kwenye michezo minne tofauti, ukiwemo na soka. Timu yetu ya soka ilikuwa vizuri sana, tulikuwa na mfungaji mmoja ambaye alikuwa balaa. Ilikuwa akishika mpira ni mpaka golini, hata akiwa mbali vipi alikuwa hakosi. Wanafunzi wengi tulidhani angeenda kujiunga na timu ya simba au yanga, kipindi hiko timu ya Azam haikuwepo. Kijana huyu mwenye kipaji hakufika popote, licha ya timu ya mpira kufanya vizuri. Tulipomaliza shule na safari yake iliishia pale.
Kwasasa nchini kuna akademi mbalimbali ikiwepo akademi ya Makongo, Simba pamoja na Azam. Azam ni moja ya timu nchini ambayo akademi yake iko vizuri, ambayo inalenga kwenye kukuza vipaji vya wachezaji ambao wanaweza kujiunga kwenye timu ya Azam juu ya miaka 18 au wakauzwa kwenye timu nyingine nchini n ahata kimataifa na hivyo kuimarisha Azam upande wa pesa lakini pia hata kwenye upande wa hadhi yao
Ni vipi TFF itawekuza vipaji hivi?
TFF kama wasimamizi wa timu za taifa za soka inatakiwa kuanzisha akademi ambayo itakuwa inachukuwa vijana haw ana kuwaendeleza zaidi.
Kila mwaka baada ya mashindano haya kuisha kikosi cha taifa kitakuwa chini ya TFF, ambako mbali na kuendeleza vipaji vyao watahakikisha pia wanafanya vizuri darasi. Kuna wanafunzi wengine ambao huwa na uwezo mdogo darasni lakini kwenye kipaji yupo vizuri sana. TFF inatakiwa kuwatafutia mpango wanafunzi hawa kupata elimu ya ujuzi mwingine; mfano vyuo vya ufundi na kuhakikisha wanaongeza taaluma nyine mbali na soka.
TFF itatakiwa ifanye mashirikiano na timu za ndani pamoja na za nje ili kukuza zaidi vipaji vya vijana hawa, ambako itatoa nafasi ya vijana hawa kununuliwa kwenye timu za ndani na hata timu za nje. Mashirikiano haya pia yatakuwa ni kwaajili ya kubadilishana uwezo, ambako vijana chini ya TFF wanaweza kwenda kufanya mazoezi ya academy ya azam au simba. Kutokana na mashirikiano ya akademi za ndani nan je ya Afrika, pia itasaidia kwa vijana hawa kwenda kupata uzoefu zaidi nje na hivyo kuimairisha kikosi chao.
Wachezaji hawa kama watanolewa vizuri wataweza kununuliwa kwenye timu za ndani, timu za nje au kubaki kwenye kikosi cha timu yetu ya taifa inayosuasua kila kukicha (hasa wanaume) na hivyo kukiimarisha vizuri kikosi chetu kikawa tishio Dunia nzima.
Zipi faida za TFF kuwa na akademi yake?
Kukuza vipaji: Lengo la kwanza la akademi hii ni kukuza vipaji vywa kuwawezesha kujiunga na timu watu wazima au kuuzwa kwenye academy nyingine au timu nyingine. Ambapo ikitokea skauti kaelewa kipaji cha mchezaji anaweza kuingia kwenye makubaliano ya kumhamisha au kumnunua mchezaji husika
Kuingiza kipato kwa kuuza wachezaji hao kwenye akademi au timu nyingine. Ikitokea kuna timu intamka mchezaji mchezaji mmoja wako, watalazimika kuingia makubalino na akademi ya TFF na hivyo kuingiza kipato kama wakifikia makubaliano ya kumuuza mchezaji huyo
Kujenga mashirikano na timu kubwa pamoja na kuongeza hadhi ya akademi. Endapo TFF itakuwa inatoa wachezaji wazuri ni dhahiri sifa ya akademi hii itasambaa na kutengeneza mashirikiano (connection) na akademi pamoja na timu za ndani n ahata nje. Jambo litakalofanya hadhi iongezeke lakini pia hata nguvu ya kufanya makubaliano iongezeke (upande wa pesa)
Kuongeza ajira nchini: Soka inazidi kutambulika kama ajira rasmi kimataifa, japo kwa sasa bado kuna kaugumu kiasi kwa mzazi kuruhusu mtoto wake afate ndoto yake ya kuwa mchezaji wa mpira. Hii ni kwasababu kwanza timu zinafanya vibaya, lakini hata maslahi pia kwa wachezaji hayaridhishi, hivyo hata kama mtoto ana kipaji kweli, mzazi anakosa mifano ya kutosha ya kuamini kweli mtoto wake naye anaweza kufanikiwa kwenye soka. Lakini kama akademi hii ikifanya vizuri na kutoa wachezaji wengi kwenye timu za ndani na nje ya nchi sit u itaongeza ajira lakini pia itaongeza Imani kwa wazazi kuwaruhusu watoto wao kuwa wachezaji wa mpira na wadau kwenye kuwekeza zaidi kwenye timu hizi.
Yote kwa yote, tuna nafasi kubwa ya kufanya michezo hii isiishie tu shuleni bali hata kukuza vipaji hata nje ya mipaka ya Tanzania. Mimi nimetolea mfano kwenye soka, lakini hili linaweza kutekelezwa kwenye michezo mingine pia, ambapo umoja wa kila mchezo ukahakikisha una akademi ya kukuza vipaji vya vijana kwenye michezo hiyo na kuwaendeleza zaidi na sisi pia tukaanza kuchukua medali za dhahabu, siyo kila mwaka tunaringia Filbert Bayi aliyetamba miaka ya 80 huko wakati tuna vijana wengi wenye vipaji wanaoweza kupeperusha bendera vzilivyo. Hii pia itapunguza mtindo wa kupeleka watu wasiyo na uwezo au kwa kujuana sababu wachezaji hawa wanakuwa wamepatikana kwa njia ambayo haina upendeleo, bali ni kipaji na uwezo wake binafsi ndio utambeba.

Upvote
3