TFF, kwanini magari yana park ndani ya uwanja wakati wa michezo ya ligi kuu?!

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262
Sijaelewa ni kwanini magari yanaruhusiwa kupark ndani ya uwanja wakati wa michezo ya ligi kuu. Wakati wa mchezo wa Yanga na Lipuli kule Iringa uwanja wa Samora niliona zaidi ya magari 11 likiwemo basi yapo ndani ya uwanja tena mbele ya majukwaa ya watazamaji. Sasa hivi naangalia mechi ya Alliance na Yanga uwanja wa Kirumba naona magari kibao ndani ya uwanja yakiwemo mabasi tena mengine yamepaki nyuma ya goli.

Hivi haya magari ni ya nini uwanjani? Na yenyewe yanaangalia mpira? Je yanalipa kiingilio? Je hakuna nafasi za kupaki nje ya uwanja? Ni kwanini mnaweka magari mbele ya watazamaji? Mbona mambo kama haya kwenye ligi za wenzetu kama Uingereza, Italy, Spain na Ujerumani hatuyaoni? Au kuna watu wanataka wanapoangalia mpira na magari yao nayo yawe yanaangalia na wenyewe.wawe wanayaona?

Mimi nashauri mtindo huu wa kishamba kabisa uachwe magari yote yapaki nje ya uwanja hata lile la wagonjwa lipaki standby kwenye mlango wa kuingilia siyo ndani kwakuwa yanaharibu mandhari ya uwanja na kuwanyima watazamaji uwazi wa kuona mpira vizuri. Hata wanaoangalia kwenye TV wanataka kuona mpira siyo magari au pikipiki.

Kuna siku mtindo huu utakuja kuleta madhara makubwa hasa ikitokea vurugu, ajali au mchezaji anaweza kufumua shuti kali likatoka nje hadi kuvunja vioo vya vimeo husika. Nashangaa ni kwanini mtindo huo wa kijinga unaonekana kwenye viwanja vya mikoani tu lakini uwanja wa taifa, uwanja wa uhuru na nadhani uwanja wa Mkwakwani Tanga huwezi kuona ushamba huo.

Nawasilisha!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…