TFF mkimsamehe au kumpunguzia adhabu Manara na wale wengine mliowafungia waachiwe

Sir robby

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2022
Posts
2,396
Reaction score
4,080
ANGALIZO kwa TFF
Endapo TFF inakubali Kula Matapishi yake kwa Kuwasikiliza Wanaoshabiki UHUNI na MATUSI ya HAJI MANARA tunaitaka TFF iwajibike kwa kuwaondolea Adhabu na kurudisha Fedha za Faini walizotozwa Watu mbalimbali waliohukumiwa na Kamati ya MAADILI ya TFF.Tunawasikia Watu mbalimbali wakimtetea Haji Manara badala ya kumkemea kwa Tabia mbaya aliyonayo.Haji Manara wakati akiwa Msemaji wa SIMBA Rais wa TFF MALINZI alimfungia kupitia Kamati ya Maadili ya TFF na huyu RAIS wa Sasa wa TFF Bw. KARIA ndiye alimsamehe lakini leo tena Karudia hivyo ni MZOEFU .Wafuatao Wamefungiwa na Kamati ya Maadili wanatumikia ADHABU zao je MANARA yeye ni nani mpaka Asitumikie?
1.Shafii Dauda kafungiwa Miaka 5
2 Lwitiko wa Mbeya kafungiwa Miaka 10
3.Mbwana Makata kafungiwa Miaka 5
4.Michael Wambura kafungiwa Miaka 5
5.Kiongozi wa Klabu ya Buashara United kafungiwa MAISHA
Watanzania Tunataka Heshima kwenye SOKA sio UHUNI wa Manara
na Viongozi wa Vilabu na Wazee wa YANGA badala ya kumkanya MANARA eti mnatishia kwenda kumwona RAIS na Klabu ya YANGA badala ya kumkanya Msemaji wenu Eti mnadai umefungiwa YANGA
Watanzania Hatutaki UHUNI kwenye SOKA LETU
MANARA atumikie ADHABU Kama WENGINE hakuna aliye juu ya SHERIA
 
Tuache undumila kuwili Haji anakera na kuudhi watu wengi hastahili kabisa kupunguziwa adhabu Tena ingefaa aongezewe iwe fundisho kwake na wengine wasio na lugha ya staha
 
TFF wakimfungulia, basi kila atakayefungiwa baada ya hapo, watu wake wataandamana kudai afunguliwe..
 
Wanawashwaaa walee kwanza siyo wazee wale ni kikundi cha wanywa kahawa pale Jangwani
 
Angekaa kimya au kuonyesha utulivu ingekua rahisi kumpunguzia adhabu lakini mtu mwenyewe mdomo mchafu bado anabwabwaja.
 
Haji siyo wakuachwa afungishe maisha kabisa

Mm n mwana yanga ila nimefurah Sana huyu bwana kufungiwa

Gsm waache kutuchukulia poa ss mashabiki sikatai wamewekeza ila kumleta mtu aliyetutukana miaka yote ilikuwa dharau kubwa Sana
 
Fungia ,fungulia ni kazi ya shetani,kwahiyo wewe ni mfuasi wa shetani?

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Tatizo la watu wengi Sana mko emotional...yaani mnaweka emotions zenu kwenye Jambo la kisheria...swali la kwanza hizi sheria ziko fair ..swali la pili .. utaratibu uko fair?...swali la tatu Haji anatakiwa kuadhibiwa au kukomolewa na kukomeshwa?...je kazi ya TFF ni nini?wanafaidika nini Haji akifungiwa?wanapata hasara IPI?
 
Haji siyo wakuachwa afungishe maisha kabisa

Mm n mwana yanga ila nimefurah Sana huyu bwana kufungiwa

Gsm waache kutuchukulia poa ss mashabiki sikatai wamewekeza ila kumleta mtu aliyetutukana miaka yote ilikuwa dharau kubwa Sana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sema wee wa upande wake, labda watakuelewa.
 
Hoja sio haji kufunguliwa au kupunguziwa adhabu,bali karia nae afungiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…