TFF, Mo'29, Jasmine na Jemedari

Joined
Jan 3, 2020
Posts
16
Reaction score
41
Ni aibu kwa TFF kuwa sehemu ya uharamia wa soka Tanzania.... Patrick Nyembera alimhoji Fiston Mayele akiwa kwenye kambi ya Simba Cairo, Nyembera ni mnazi wa simba inajulikana Mayele anawakilishwa na wakili msomi Jasmine Rasack ambaye anamwakilisha na Feisal Salum.

Hivi karibuni kumekuwa na tabia ya wachezaji wanaowakilishwa na wakili msomi Jasmine kuisema YANGA vibaya timu iliyouza na kupandisha thamani zao Afrika na Tanzania ...

Kauli za Mayele zilifutwa na Azam TV kwa kuwa na maudhui potofu kuhusu YANGA na hata nchi, la kustaajabisha hakuna aliyehoji kwanini Mayele ayaongee yale kwenye kambi ya Simba kama hakufadhiliwa na wenyeji wake kambini humo?

Mayele siku zote anakiri anatafuta hela kwa muktadha huu Mayele hawezi kuhojiwa bila mafao inamaana alilipwa kuyasema yale ndani ya kambi ya Simba.....

Feisal alitumika sana kutoa kauli kuidhalilisha YANGA kila ilipokua na mechi ngumu au ya mtoano km ambavyo Mayele anafanya siku hizi ...la kustaajabisha TFF kwa muda sasa imekuwa ikitoa maamuzi ya kuiadhibu YANGA katika muda mfupi sana na maamuzi yatamuhusisha refa kama tofauti ya goli ni moja.

Refa aliyeruhusu goli la Max Nzengeli dhidi ya Ihefu hakuadhibiwa au kukosolewa kwasababu tofauti ya magoli ilikuwa kubwa yote haya TFF inayafanya kutoa taswira YANGA inabebwa mbali ya hayo taarifa za kufutwa kadi nyekundu ya Lameck Lawi imefutwa iljali mechi ya Namungo dhidi ya YANGA Aucho alipewa kadi lakini kwa kalamu ya Jemedari Saidi kuhusu kadi ile kamati ikaamua kumfungia Aucho aliyeadhibiwa na refa wa mchezo lakini kamati hiyo hiyo ilikataa kuwafungia John Bocco, Clotus Chama kwa maelezo kuwa waliadhibiwa kwa kadi na refa wa mchezo.

TFF imekuwa ikitoa habari mbaya za YANGA hata kabla ya YANGA wenyewe kuzipata, mfano sakata la Kocha Luc Eymael taarifa iliipata Jemedari Saidi kabla ya walengwa YANGA kutoka kwa Katibu Mkuu wa TFF, kuhusu YANGA kufungiwa usajili na CAF mpaka wamlipe Eymael stahiki zake, ingawaje TFF iliipiga faini YANGA kuhusu kauli za kocha Eymael lakini haikupeleka ushahidi wakel huo CAF na YANGA ikapigwa faini tena na CAF kwa kumfukuza kocha aliyeadhibiwa na TFF kwa kauli ya kibaguzi ... Leo TFF imetoa adhabu ya faini kwa YANGA na simba na kuifuta kadi ya Lameck kabla ya mchezo wa YANGA dhidi ya Tabora United.

Kulikua na haraka gani ya kutoa uamuzi huo leo tena siku ya Mei Mosi na siyo baada ya Mechi kuchezwa kesho? Tofauti ingekua ni nini km nia ya TFF si kuleta taharuki kwa YANGA kabla ya mechi zake km Mayele alivyohojiwa kwenye kambi ya simba Misri kabla ya mechi ya YANGA na Mamelodi, Mayele anajua habari mbaya zinawaathiri vipi wachezaji wa YANGA ndio maana alifanya vile kwasababu alikuwepo YANGA wakati Feisal anadhalilisha timu...wakati Barbara akiwa simba alifanya ya Mayele akiwa Africa ya kusini kwa kuichafua YANGA ...baada ya habari za Nyembela kuondolewa na Azam TV.

Jemedari Saidi alikasirika sanaaa na hata kufikia kumwita Dastan Tido Muhando "MWOGA" Mwandishi aliyetoa breaking newz ya kuuawa kwa Robert Auko.,...TFF iache kuwa sehemu ya mbinu chafu
 
Thread imejaa hoja zenye akili mwanzo mwisho, Karia na TFF yake hawezi kujibu hata moja!

Mkuu, umeandika sana. Hats off!
 
jasmine sio wakili msomi na wala hana taaluma ya sheria
 
Mkuu ukiona unapondwa Sana ujue umewazidi wenzio vitu vingi by the Acha waseme sisi hao tunapeta....

ACHA WAFU WAZIKANE
 
Mkuu sijaelewa MO29 ameingiaje? Hao wengine Iko wazi kwamba Yanga ni kama mtaji kwao, hivyo wanafosi wapate Cha kuiongelea ili wapate kula.
 
Yule Rais wa Shirikisho na wahuni wenzake mwisho wa uongozi wao ni lini?
 
TFF ya Karia imejaa unazi kuliko utendaji, Katibu mkuu pale TFF na karia ndiyo virus kubwa ya mpira wa Tanzania
 
Huyo kitambi msimalia .... Acha amalizie muda wake... Mkakakati uliopo no hawezi kurudi Tena hapo Tff hivyo acha afanye anachoona ni sahihi...kila Zama na kitabu chake..... Miala ya msomali Simba wamekuwa watoto wema uchaguzi ujao ni zamu ya yanga kuweka mtu wake.... Iwe jua iwe mvua. Na mipngo imeshaiva ni Dr fulani yupo taasisi moja...
 
Yaani timu Yaani timu ikisemwa vibaya unaumia kabisa? Au sijaelewa?
 
Ukweli mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…