TFF na Bodi ya ligi endeleeni kujitekenya na kucheka wenyewe lakini tambueni Azam kipigo kipo palepale

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Mara mbadilishe tarehe, Mara mbadilishe uwanja mna kaa tena mnakumbuka kitu mnarudisha mechi ichezwe kwenye uwanja ulioibadilisha mwanzo.

Kiufupi mnajitekenya na kucheka wenyewe.

Je, tukisema mnapanga njama za kuihujumu Yanga Sc ipoteze dhidi ya Azam tutakua tumekosea!?

Hangaikeni mnavyoweza Tena ikibidi mechi ipelekeni hata mwezini na Yanga haitoathirika kisaikolojia Kama mlivyokusudia Azam atapigwa kipigo kibaya tu.
 
Hiyo bodi sidhani kama wanakaa kikao kufanya maamuzi yao ya hovyo hovyo kila kukicha naona kama wanapigiana simu tuu na hawajui kuwa haya mashindano yana Udhamini mkubwa wao wanafanya vitu hovyo hovyo tuu..
 
Sidhani kama kuna Mashindano ya anayeanzisha nyuzi nyingi humu,kiazi kweli wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…