44mg44
JF-Expert Member
- Jun 16, 2019
- 2,158
- 2,186
Naanza kwa kurejea mechi ya Yanga na Azam, hii mechi ilionesha wazi kuwa kuna rushwa kwa waamuzi. Mpira kuna kipind ulitoka nje kabisa halafu mchezaji wa Yanga akakimbilia na kuurejesha uwanjani hatimaye wakafunga goli ambalo si halali yao. Pia Azam walipata penati wakanyimwa, haya yote yanasababisha tunapata bingwa asiyestahili kabisa.
Kama inawezekana TFF iichunguze vizuri hiyo mechi ya Yang na Azam ione makosa hayo ya wazi kisha Yanga wapokonywe point.
Ligi ikiendeshwa vizuri pasipo na upendeleo wowote, pia rushwa ikakomeshwa tutapata bingwa halali na atatuwakilisha vyema kimataifa.
Ni aibu kubwa sana kwa timu ngeni kuja kutufungia nyumbani. Tujirekebishe pia tuamke, wakat ni sasa.