TFF ndiyo wanamiliki soka hapa nchini?

TFF ndiyo wanamiliki soka hapa nchini?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Nimesikia TFF wamemfungia Shafii Dauda kujihusisha na soka ndani na nje ya nchi kwa miaka mitano. Imekuwa ikifungia watu wengi sana. Naomba kujua kama TFF wana monopoly ya soka nchi, yaani kama TANESCO walivyo na monopoly kwenye kuzalisha na kuuza umeme? Kwamba ukitaka kufanya shughuli zozote za soka ni mpaka TFF wahusike! Nani amewapa mamlaka hayo, ni halali kuwa hivyo?

Hivi mtu hawezi toka huko akaanzisha kampuni/taasisi yake. Akaanzisha ligi yake bila kujihusisha na hao TFF? Je kunaweza kuwa na vyama na mashirikisho mengi ya soka ambayo hayahusiana na TFF, CAF na FIFA?
 
Tff ndio baba wa soka Tanzania hao wengine tumewa-follow tu.
 
Nimesikia TFF wamemfungia Shafii Dauda kujihusisha na soka ndani na nje ya nchi kwa miaka mitano. Imekuwa ikifungia watu wengi sana. Naomba kujua kama TFF wana monopoly ya soka nchi, yaani kama TANESCO walivyo na monopoly kwenye kuzalisha na kuuza umeme? Kwamba ukitaka kufanya shughuli zozote za soka ni mpaka TFF wahusike! Nani amewapa mamlaka hayo, ni halali kuwa hivyo?

Hivi mtu hawezi toka huko akaanzisha kampuni/taasisi yake. Akaanzisha ligi yake bila kujihusisha na hao TFF? Je kunaweza kuwa na vyama na mashirikisho mengi ya soka ambayo hayahusiana na TFF, CAF na FIFA?
Mkuu ni kweli adhabu wanazotoa TFF ni za uonevu mkubwa tena hasa TFF ya Wallace Karia

Lakini kwa upande mwingine TFF ndio wenye mpira wao. Yaani ni kama monopoly juu ya uongozi wa soka.

Huwezi kuandaa mechi za soka bila kibali chao. Kama ambavyo FIFA wanawavyoweza kuamua lolote, nchi yoyote bika kuingiliwa na serikali yoyote isipokua kwa issue za kijinai
 
Umeuliza jambo la maana sana.
Mchezo wa soka ni mchezo wa hiari na hauna hati miliki ya mtu au taasisi yoyote. TFF kumfungia mtu asijihusishe na soka huko ni kuingilia haki na uhuru wa mtu binafsi unaotajwa kikatiba.

TFF inaweza kumzuia mtu asijihusishe na michezo ya soka inayoratibiwa na TFF na sio kumzuia mtu asijihusishe na soka.
 
Sababu ya Shafii kufungiwa ni Nini kwani?

Nakumbuka ni miongoni mwa Watangazaji wa Sports Extra ya Clouds Fm, it means hatotangaza Tena au..?
 
Mkuu ni kweli adhabu wanazotoa TFF ni za uonevu mkubwa tena hasa TFF ya Wallace Karia

Lakini kwa upande mwingine TFF ndio wenye mpira wao. Yaani ni kama monopoly juu ya uongozi wa soka.

Huwezi kuandaa mechi za soka bila kibali chao. Kama ambavyo FIFA wanawavyoweza kuamua lolote, nchi yoyote bika kuingiliwa na serikali yoyote isipokua kwa issue za kijinai
Mkuu, FIFA haina hati miliki na mchezo wasoka na wala haina mamlaka ya moja kwa moja na kila mchezo wa soka unapochezwa duniani. Yapo mashindano mengi ya soka duniani yanafanyika na hayana uhusiano wowote na FIFA na katika mashindano hayo FIFA haiwajibiki chochote katika uratibu au usimamizi wa hilo soka.

Kumbuka kuwa sio kila nchi ni mwanachama FIFA, nchi kuwa mwanachama wa FIFA ni jambo la hiari na kuna vigezo na masharti kuwa mwanachama wa FIFA, na kama nchi sio mwanachama wa FIFA haiwajibiwi au kufaidika na FIFA.

Mwisho, nikukumbushe tu, mara kadhaa nchi fulani ziliwahi kufungiwa na FIFA, hii iliwanyima fursa ya kushiriki mashindano yanayotambulika na FIFA lakini wananchi wa nchi husika waliendelea kusakata soka kama kawaida.
 
Umeuliza jambo la maana sana.
Mchezo wa soka ni mchezo wa hiari na hauna hati miliki ya mtu au taasisi yoyote. TFF kumfungia mtu asijihusishe na soka huko ni kuingilia haki na uhuru wa mtu binafsi unaotajwa kikatiba.

TFF inaweza kumzuia mtu asijihusishe na michezo ya soka inayoratibiwa na TFF na sio kumzuia mtu asijihusishe na soka.
Sasa sijui umeandika nini, kwani kuna mchezo wa soka ambao utaendeshwa bila kuratibiwa wa Tff?.. Hiyo itakuwa ni ndondo aka cha ndimu aka dogoli
 
Shukran kwa darasa zuri Mkuu. Nimeelewa
 
Umeuliza jambo la maana sana.
Mchezo wa soka ni mchezo wa hiari na hauna hati miliki ya mtu au taasisi yoyote. TFF kumfungia mtu asijihusishe na soka huko ni kuingilia haki na uhuru wa mtu binafsi unaotajwa kikatiba.

TFF inaweza kumzuia mtu asijihusishe na michezo ya soka inayoratibiwa na TFF na sio kumzuia mtu asijihusishe na soka.
Ajabu kabisa. TFF wanaweza zuia mtu asijihusishe na mipira wanaoratibu wao au vyama vinavyounda shirikisho lao. Lakini hawana hati miliki ya mpira. Na hawana haki ya kumzuia mtu kuorganise masuala ya mpira nje ya taasisi yao.
 
Sasa sijui umeandika nini, kwani kuna mchezo wa soka ambao utaendeshwa bila kuratibiwa wa Tff?.. Hiyo itakuwa ni ndondo aka cha ndimu aka dogoli
TFF ndiyo wanataka uamini hivyo. Kwamba bila kupita kwao hakuna soka.
 
Back
Top Bottom