TFF, NHIF zasaini mkataba

TFF, NHIF zasaini mkataba

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Mwesigwa Selestine leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja na mfuko wa huduma ya afya (NHIF) kwa ajili ya kutoa huduma kwa wachezaji wa Ligi Kuu pamoja na viongozi wa benchi la ufundi.

Hafla ya kusaini mkataba huo imefanyika katika hoteli ya Protea Courtyard iliyopo Upanga jijini Dar es salaam ambapo katibu mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF Rehani Athumani walisaini kwa niaba ya pande hizo mbili.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa uwekaji sahihi mkataba huo, Mwesigwa amesema anaishukuru NHIF kwa kudhamini kutoa huduma ya afya kwa wachezaji na mabenchi ya ufundi kwa vilabu vyote 16 vinavyoshiriki Ligi kuu ya Vodacom.

Aidha Mwesigwa ameviomba vilabu vya Ligi Kuu nchini kutoa ushirikiano na watoa huduma ya afya kwa wachezaji na viongozi kutoka NHIF pindi watakapokuwa wanafika kwenye vilabu vyao kwa ajili ya shughuli mbalimbali.

Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Rehani Athumani akiongea kwa niaba ya mfuko huo amesema wako tayari kufanya kazi na kutoa huduma ya afya kwa ngazi zote ikiwemo kwa timu za madaraja ya chini pia.

TFF na NHIF zimeingia mkataba wa mwaka mmoja wa udhamini wa huduma ya afya kwa wachezaji kwa ligi kuu na viongozi wa benchi la ufundi, mkataba ambao unaeza kuongezwa kila unapomalizika.

TFF kwa kupitia bodi ya ligi inavitaka vilabu vyote vya Ligi Kuu vitoe ushirikiano kwa wafanyakazi wa NHIF katika kurahisiha shughuli za usajili ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa na nyaraka sahihi zikiwemo picha za wahusika katika muda sahihi.
 
Wazo zuri lakini NHIF imeanza kuingiwa "utanzania" Pale Tumaini Hospital booking za kuwaona madaktari bingwa hupewa number kuanzia 11. Za mwanzo 1 mpaka 10 ni kwa watu wa cash!
Mchezaji aliyeumia kwa maana hiyo atahudumiwa baada ya wale wa cash.Najua hilo ni tatizo la Hospital na si NHIF. Inabidi walijue na kulifanyia kazi. Hospital zenye tabia hizo waziondoe kama walivyofanya kwa Agha Khan.
 
Wazo zuri lakini NHIF imeanza kuingiwa "utanzania" Pale Tumaini Hospital booking za kuwaona madaktari bingwa hupewa number kuanzia 11. Za mwanzo 1 mpaka 10 ni kwa watu wa cash!
Mchezaji aliyeumia kwa maana hiyo atahudumiwa baada ya wale wa cash.Najua hilo ni tatizo la Hospital na si NHIF. Inabidi walijue na kulifanyia kazi. Hospital zenye tabia hizo waziondoe kama walivyofanya kwa Agha Khan.

Bado naona umuhimu wa Ujamaa, watu wachangie huduma lakini zitolewe na Serikali tu, Serikali! Watu binafsi wakiendesha huduma muhimu za afya na elimu unazalisha ubora mwingi unaoumiza na kuwapa faida kubwa, wanajifanya wanaali wagonjwa lakini ni wepesi kupeleka mtu kwenye upasuaji kwa kuwa unalipa.

Serikali itoe huduma za afya!
 
Back
Top Bottom