Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kuwa klabu ya Yanga imekamilisha taratibu zote za kumtumia Abdihamid Moallin kama kocha msaidizi namba mbili wa kikosi chao ambapo ameanza kutambuliwa kikanuni katika mchezo wa leo Desemba 29 dhidi ya Fountain Gate.
Vilevile Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imemuonya vikali Moallin kwa kosa la kuketi kwenye benchi la ufundi la klabu hiyo katika michezo mitatu (3) ya Ligi Kuu kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:17 ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za Mchezo.