TFF someni hapa, Ila Kumwembe ajiandae kwa huyu dogo yupo vyema sana

Alegria do povo

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2013
Posts
293
Reaction score
441
SASA NIMEAMUA WAJUKUU ZANGU NITAWASIMULIA KUHUSU NYERERE.

Nimetamani sana hapo kwenye Makala yangu ya leo Jumapili ya Tarehe 5 June ingesomeka TFF ITAMBUENI TOFAUTI YA MAVAZI na sio Mbeya City kama ilivyosomeka. Anyway tabia hii ya kufuta vumbi nguo zionekane safi itaisha lini? Hatujaamua tu kuzivua kisha tuzifue? TFF naomba mkasome programme iliyofanywa na Serbia baada ya kuona soka umekuwa mchezo wa nne kwa kufuatiliwa na kuchezwa na vijana nchini mwao.

Serbia wana programme inaitwa My School, My Club. " l

MY SCHOOL - MY CLUB

Being inspired by the idea that a lot of children and youth population play football, the Football Association of Serbia has created a project called "My school - My club!" whose implementation is supported by UEFA, the Ministry of Education, the National Office of the President of the Republic of Serbia and the numerous media partners"

Uingereza wana programme inaitwa Football at the Heart of school level. " This can be achieved through The FA Secondary School Programmes, which is football’s lasting commitment to providing schools with child friendly programmes, high quality services that schools value, while actively engaging with teachers to ensure we complement their work".

Kule German walivyofanya vibaya 2000 kwenye Euro wakabadili uongozi na kuwekeza kwenye vijana. Ambayo program iliitwa DFB Talent Development Programme.

"More than half of those players came through the DFB's talent development programme, which was introduced in 2003 with the aim of identifying promising youngsters and providing them with technical skills and tactical knowledge at an early age. Covering 366 areas of Germany, this impressive initiative caters for children aged 8 to 14 and is served by 1,000 part-time DFB coaches, all of whom must hold the Uefa B licence and are expected to scout as well as train the players. "We have 80 million people in Germany and I think before 2000 nobody noticed a lot of talent," Dutt says. "Now we notice everyone."

Hii programme kufikia mwaka 2012 ndio ilizalisha akina Julian Draxler (19), Andre Schürrle (22), Sven Bender (24), Thomas Müller (23), Holger Badstuber (24), Mats Hummels (24), Mesut Ozil (24), Ilkay Gundogan (22), Mario Götze (20), Marco Reus (23), Toni Kroos (23) kipindi hicho umri wao.

Yaani ni miaka 12 baadae wakapata kizazi cha dhahabu na baada ya hapo miaka 2 baadae wakatwaa kombe la dunia.

Sisi tumerogwa? Mzee mwinyi achinjiwe kondoo basi kama kweli laana yake ilitushika anywe damu ile. Inawezekana vipi mashuleni, vyuoni na katika taasisi mbalimbali mnafundisha maendeleo na hakuna project za msingi zinazozalishwa kutokana na vijana hawa. Hakuna watu wanaofikiria kweli.

Inauma kuona Mbunge Zitto Kabwe anamwonyesha Waziri mwenye dhamana ya michezo kuwa katika hotuba yake hakuna sehemu yoyote kataja timu ya Taifa. Maana yake hakuna kipande chochote ambacho kinaashiria majaliwa ya Nchi hii katika sekta hii.

Kama Soka limetushinda wenzetu Spain sasa wanahamia kuhakikisha Basketball inakomaa kama marekani maana huku washaweka misingi inayojiendesha. Tennis walishamaliza muda mrefu sana na wanao akina Muguruza sasa hivi.

China hawapendi soka lakini wameamua tu kuupa kipaumbele. Gibraltar ina mpango kabambe baada ya kupewa ruhusa ya kuwa mshiriki kamili wa Uefa.

Hivi ni mpaka siku Watanzania waingie na jezi za Nigeria tukiwa tunacheza nayo ndo itambulike kuwa tunatakiwa kubadilika? Umissetta, Copa CocaCola, Uhai, Rollingstone, Umitashumita hivi vyote vilikuwepo kwa lakini ni sawa na kipofu alikabidhiwa usukani darajani. Nchi imetumbukia mtoni.

Inawezekana viongozi wetu hawajui labda wengine wanafanyaje acha tuwawekee basi hata majina ya programme za wenzetu. Maana serikali imekopa mifumo mpaka ya Big Results now. Tanzania ndio nchi pekee na jirani zetu kadhaa ambao maana ya siasa ni dhambi dhidi ya wenyewe kwa wenyewe na sio baraka ya kutafuta maendeleo. Ndio maana ikitajwa siasa ni kama Tusi. Kila linalofanywa baya maelezo yake ni kuwa siasa imeingilia. Kweli hii?

Inaniuma sana kwa sababu Inawezekana kabisa athari ninazozipata kama Mtanzania zitanifanya wajukuu zangu niwasimulie zaidi kuhusu TFF kuliko Mlima Kilimanjaro, Mchanga unaotembea, Tanzanite, Ngorongoro Crater, Olduvai na Serengeti. Lakini hata hivi vinaweza visiwe na maana maana havina faida inayokusudiwa zaidi Wakenya ndio wanafaidika nayo. Uwanja wa Taifa unafurahisha kukiwa na matamasha kuliko mechi na TFF imehusishwa kupanga matokeo.

Nitawasimulia Wajukuu kuhusiana na Mwalimu Nyerere. Wala hakupenda soka saba lakini Alitupa uhuru, na kipindi akiwa hai bado na nguvu zake tukashiriki Mataifa ya Africa na alitufanya tupendane sana. Siku hizi Injinia ndo anatafsiri Sheria. Tanzania ni ya mwendokasi. Sitohuzunika tena naahidi.

Mtag mwenye mapenzi ya dhati na nchi hii.

Nicasius Nicholaus Agwanda (Coutinho Suso )
 
Sio Edo Kumwembe ajiandae...Edo ni Legend inabidi awe karibu na huyo dogo ampe madini zaidi ili aweze mkali hapo mbele kumwembe atapopumzika katika uandishi
 
Eti sikuhizi injinia ndio anatafsiri shelia. hahaha!
 
suso jamaa angu sana,na anajua kuchambua mpira.kwa edo atasubiri kidogo.
 
Edo kumwembe niwa kipekee kabisa yaani usimfananishe na hao wengine
Binafsi napenda status zake huwa anaandika kimasihara ila zinakuwa na ujumbe ndani yake
 
Huwezi kulinganisha hiyo makala na za Edo. Huyo dogo bado sana. Wengi wanajaribu kumwiga Edo,akiwepo huyo dogo,lakini hamna kitu.
 
anajtahidi, Edo anachungulia sana mtandao.
 
Kumwembe Edo jamaa anajua hadi anaudhi bwana..... Kuna mda huwa anapost vitu Fb aisee ni kwa ufupi lakini ujumbe mzito sana..... Wingine wasuburi kwa Edo
 
Amekosea tu kusema China haipend football

mashabiki wengi wa ligi ya Uingereza wanatoka China
 
Edo is genius, japo kuna mambo mengine huwa sikubaliani naye lkn jamaa yuko vizur

Inafurahisha mtu kuandika kile ambacho wewe ulikuwa ukifikiria
 
Huyu chalii namfahamu....
Kwa kifupi yupo Overrated but na appreciate effort yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…