TFF taa za uwanja wa mkwakwani ni hafifu, rekebisheni kabla mambo hayajaharibika

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Nimewasili Tanga jioni kwenda kumshuhudia Che Malone ukuta wa Yericko pamoja na fundi wa mpira Fabrice Ngoma kwenye gemu ya ngao ya hisani tarehe 10 vs Singida, sasa hivi niko Mkwakwani naangalia mechi ya kirafiki baina ya Coastal Union vs Singida, uwanja ni mzuri sana, nyasi zimekolea ukijani hadi ng'ombe wanazitamani.

Shida nayoiona ni uhafifu wa taa, kucheza wanacheza lakini vivuli vya wachezaji vinaonekana jambo ambalo linaashiria kuwa taa hazina nguvu ya kutosha, TFF rekebisheni hali hii ili wale wenye chuki na nyie wakose la kusema.

Mtakuja kunishukuru
 
Tutawaambia mashabiki wawashe tochi za simu zao.
Usijari mkuu na asante kwa kujali.
 
Nina wasiwasi mkubwa na akili za watu wote waliopendekeza hayo mashindano kufanyika kwenye uwanja wenye pitch mbovu, halafu usiku!
 
Nadhani wamekusikia na ninawaelekeza walifanyie kazi haraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…