TFF: Tanzania kuwa na timu 4 mashindano ya CAF msimu ujao

TFF: Tanzania kuwa na timu 4 mashindano ya CAF msimu ujao

Kifurukutu

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2013
Posts
4,641
Reaction score
6,694
Hatimaye yametimia!

Ongezeko la timu nne kushiriki mashindano ya CAF msimu ujayo yamekuja baada ya mafanikio ya SIMBA SC kufanikiwa kufika robo final licha ya kutolewa na Kaizer Chiefs ya South Africa.

CAF champions league itashirikisha mshindi wa VPL kama ilivyo kawaida yake, huku mshindi wa pili pia akipewa chapuo la kubebwa na mafanikio ya Simba kushiriki michuano hii mikubwa barani Africa.

Aidha, Mshindi wa fainali ya FA atakwenda kushiri michuano ya CAF shirikisho na mshindi wa pili pia atapata nafasi hiyo.

Incase bingwa la VPL ndiye atakayekuwa mshindi wa FA, msimamo wa VPL utatumika kupata wawakilishi wa Tanzania kimataifa, nafasi ya tatu itapewa nafasi.

Haya yamewekwa wazi na CAF kwamba Tanzania imepanda kwa kujizolea point za kutosha kutokana na Mafanikio ya SIMBA SC.

Hii inaonesha jinsi gani SIMBA ndiye baba na mama wa soka hapa nchini, imekuwa kawaida kuvibeba vilabu weak kushiriki michuano hii muhimu Africa.
 
Back
Top Bottom