TFF, toeni maelezo kwanini Baraka Kizuguto anatuhumiwa kwa kuibeba timu kongwe kuhusu usajili wa under 20

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Tuhuma zinasambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa BW Baraka Kizuguto ambaye aliwahi kuwa msemaji wa Yanga na sasa ni mmoja wa maafisa wa TFF anayeshughulikia masuala ya club licensing akilalamikiwa kuwa aliihujumu Simba kwenye mchezo dhidi ya Al ahly kwa kuipa upendeleo Al ahly badala ya Simba.

Inasemekana pia juzi Simba under 20 wamegoma kucheza na under 20 ya Yanga kwa madai kuwa under 20 ya yanga ilichelewa kufanya usajili hadi dirisha linafungwa na madai yanasema kuwa jamaa huyo ambaye ni Yanga lia lia na ameshindwa kutofautisha kati ya kazi na mapenzi ameisaidia utopolo kuvunja kanuni ili kuiepuka yanga isishushwe daraja maana ili uweze kucheza ligi kuu kanuni zinataka uwe na under 20.

TFF isipuuze madai hayo, tujenge utamaduni wa kuwajibishana na hawa watu wanaoendekeza mapenzi katika kazi wekeni pembeni wanaharibu taswira ya taaasisi.
 
Tatizo la tff ni kuamini hawawezi kupata viongozi wengine bila kuchukua waliopitia Simba au yanga.
Yanga wamezoea kubebwa Ila wakikaziwa wanaanza kunyooshea watu vidole kuwa Simba. Dirisha la usajili wa timu za vijana unajulikana, wameshindwa Nini kuzingatia huo muda?
Wafate kanuni, Kama walivyogomea mechi ya Simba kwa madai ya kuvunjwa kanunu ndivyo TFF inatakiwa kuwashusha daraja kwa mujibu was kanuni.
 
Bongo kuna timu zinaamini haziwezi kuguswa na ndio sababu unaona watu wanafanya wanavyojisikia
 
Mbumbumbu acheni kulia lia. Wallace Karia mbona ni mdau wa timu yenu, lakini hatusemi?

Mnafikiria timu kama Yanga (Bingwa mtetezi) inaweza kushushwa daraja kirahisi tu, na kwa sababu za kipuuzi kama hizo!! Mtasubiri sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…