kingphisher
Member
- Nov 30, 2024
- 45
- 79
Hii soka inaelekea wapi? TFF imekiri wazi kuwa ile kadi nyekundu aliyopewa mchezaji wa Namungo haikuwa sahihi, lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya maamuzi mabovu ya mwamuzi. Hivi hii inaleta taswira gani?
Mwamuzi alikuwa na makosa mengi, hasa kwa upande wa Namungo. Alikuwa makini mno kuhakikisha goli la Namungo halifungwi wakati Simba wanashambulia, kiasi kwamba kosa dogo tu kutoka kwa Namungo lilitosha kupewa kadi au faulo. Hii ni haki kweli?
TFF haijasema chochote kuhusu faulo ya wazi ambayo Namungo walinyimwa, wala makosa mengine mengi ya mwamuzi. Upuuzi huu utaisha lini? Mwamuzi anatoa kadi anavyotaka, kana kwamba hakuna sheria yoyote ya kufuata, halafu TFF inaangalia tu kama vile hakuna kilichotokea. Sasa hiyo kadi mliyoifuta inamsaidia nani? Mnaelewa madhara ya kadi nyekundu kwa timu? Mnajua namna inavyobadilisha mchezo? Hivi nyie... mmeniudhi sana!
Kila siku Simba wanacheza na marefa na hamuoni!
Mechi ya Simba na Mashujaa, Mashujaa wanapiga kona, mpira haujafika golini, mwamuzi anapuliza filimbi ili kuzuia goli!
Mechi ya Simba dhidi ya Namungo mzunguko wa kwanza, Simba anaongoza 2-0, Namungo wanarudi mchezoni hadi 2-2, wanapata nafasi ya kufunga goli la ushindi, refa anamaliza mpira ghafla! Hizi penalti za Simba ndo usiseme! TFF, mnaharibu ligi kabisa! Kama hamuwezi kazi, nafasi hizo hazikufai!
Halafu hili suala la udhamini wa GSM! Kila siku kelele kwamba "GSM anaharibu ligi" kwa sababu Simba anapata matokeo mabovu huku Yanga anashinda! TFF inajua kabisa udhamini wa aina hii ni halali na sheria inaukubali, lakini mmekaa kimya badala ya kutoa elimu kwa wasiojua biashara ya uwekezaji na sheria zake! Mnatulia tu huku ujinga unaenezwa kila kona!
Hawa watu kama Kisugu, GB 64 na wazee wa Simba wasiojua mpira wamekazana na GSM badala ya kuangalia matatizo halisi ya marefa! Na nyie mmetulia tu!
Wakati huo huo, makampuni makubwa zaidi ya GSM yamewahi kudhamini vilabu vingi bila matatizo!
Mfano:
TFF, hii ligi mnaipeleka wapi? Tunachoka!

- Red Bull (RB Leipzig na Red Bull Salzburg) – Bundesliga & Austrian Bundesliga
- Fly Emirates (Arsenal, Real Madrid, AC Milan, PSG, Benfica) – EPL, La Liga, Serie A, Ligue 1, Primeira Liga
- Etihad Airways (Man City, Melbourne City, New York City FC) – EPL, A-League, MLS
- Betway (West Ham, Levante, Alaves, Werder Bremen) – EPL, La Liga, Bundesliga
- Nike (Barcelona, PSG, Chelsea, Inter Milan) – EPL, La Liga, Serie A, Ligue 1