TFF WAJITAFAKARI JUU YA SOKA LA TANZANIA

Chunya Boy

New Member
Joined
Nov 18, 2018
Posts
4
Reaction score
2
Naweza kusema TFF imesahau majukumu yake.
Haiwezekani kila kukicha ni malalamiko kwenye taasisi hii ya kisoka.
Hebu angalia kuanzia uendeshaji wa ligi za mikoani, madaraja ya chini na hasa daraja la kwanza.
Tutabaki kuwashangilia wenzetu wa nchi jirani wakisonga mbele kisoka na sisi kubaki tumetoa macho.
Wenzetu walikaa chini na kutafakari nini tatizo, wakalitafutia ufumbuzi na leo hii wanashine.
Mfano mzuri tuwaangalie Uganda, Kenya, Nk Walijiandaa.
Shida ya nchi yetu ni kubebana tu na kuwabeba Watu wasio na sifa. Na nchi yetu hii ina watu ambao hata danadana hawawezi kupiga lakini ndiyo waliolishika soka letu na kutuharibia soka letu.
Jiulize vijana wetu kutoka mikoani wanaofanya vizuri kisoka waking'aa tu wanawabeba kisha wanawapekeka wapi?
Marefa wazuri huenda wapi?
Lakini pia tujiulize nchi zinazofanya vizuri kwenye soka la timu za taifa je wana timu zinazomilikiwa na vyama vya soka kama Tanzania jinsi ambavyo Chama cha soka hakikohowi mbele ya Simba na Yanga. Na timu hizi ndizo zinachangia kuua soka la Tanzania.
Mchezaji akizifunga timu hizi lazima wamsajili na kumfungia chumbani na yule anayekataa kujiunga na timu hizo lazima apotezwe.
Leo ndani ya timu ya Taifa kuna makundi na ukiyafuatilia Yana Usimba na Uyanga halafu leo hii mtu anasimama na kusema lazima tufuzu kwenda AFCON sijui ipi hiyo.
TFF IAMKE USINGIZINI NA IJITAFAKARI.
Na Chunya Boy
IMG_20180224_133241.jpeg
 
𝐖𝐞 𝐰𝐢𝐥𝐥 𝐧𝐞𝐯𝐞𝐫 𝐰𝐢𝐧!
 
Na Chunya Boy View attachment 940463
Ni kweli kwamba mchezaji akizifunga timu kubwa wanamsajili ila hawamtumii. Mfano Marcel Kaheza aliwika sana na Maji maji ila kwa sasa anasugua bench ila kiukweli dogo anajua sana kama huamini wamuache aende Mtibwa au Singida United.
 
Back
Top Bottom