Katika mechi ya jana ya Yanga vs Tabora utd kuna shabiki alimrushia refa msaidizi (kibendera) chupa ya maji na kumfikia mgongoni, hii ilitokea baada ya refa huyo kunyoosha bendera kuashiria kuwa goli la Dube ni offside, na camera zilionyesha wazi ni wapi chupa imetoka hivo wanaweza kuifatilia clip hiyo ili hatua za kisheria zichukuliwe na kuzidi kukuza hadhi ya ligi kuu.