TFF wanakosea katika hili

TFF wanakosea katika hili

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Ndani ya Tanzania Football Federation (TFF) kumejaa vilaza ambavyo havijui maana ya mpira na matokeo yake ni kuingia mikataba inayovuruga tamaduni na brand za vilabu vya mpira.

Tulisikia juzijuzi hapa Yanga wakigomea kuvaa nembo zenye rangi ya mtani wake, na leo tunasikia sakata jingine la Simba kugomea kuvaa nembo ya mdhamini wa watani wao.

TFF inaonekana hawajui kuwa ndani ya mpira kuna taasisi zilizojiwekea utamaduni na taswira zao na uhai wa taasisi hizi ki mpira ni kulinda tamaduni na Taswira zao mbele ya mashabiki zao.

Ni jambo la kusikitisha kuona TFF inaingia mikataba bila kuchukua tamaduni za wadau wake na kuzijadili katika mikataba wayoingia.

kwa tff inaonekana ikitokea timu moja ikajitokeza kudhamini ligi kwa sharti la timu zote kuvaa jezi zao wao wanasaini tu, timu husika ndiyo iseme hatuwezi kuvaa jezi za wenzetu.

kwa Tff inatakiwa kila mdhamini anayekuja aelezwe kuwa wadau wetu wana tamaduni na taratibu zao na hivyo mdhamini anayejikeza lazima aheshimu taratibu na tamaduni walizojijengea wadau na madai yao yasiwe yenye kuathiri utaratibu wa mdau.

TFF watambue ukiua nembo za klabu unaua mpira na mpira ukifa hauwezi kupata mdamini wa maana.
 
Back
Top Bottom