David Serikali
Member
- Mar 2, 2012
- 57
- 17

Katika kuimarisha maandalizi ya Timu ya Taifa (Taifa Stars) kuelekea katika mashindano mbalimbali ikiwemo mechi mbili za ugenini na nyumbani dhidi ya Algeria, Rais wa TFF Jamal Malinzi ameunda kamati maalum itakayoitwa "Kamati ya Taifa Stars" ambayo majukumu yake yatakua ni.
(i)Kuimarisha huduma kwa wachezaji,
(ii)Uhamasishaji na Masoko,
(iii)Kuhamasisha wachezaji,
(iv)Kuandaa na kusimamia mkakati wa Ushindi.
Kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Farough Baghouzah, Teddy Mapunda (Katibu), huku ikiwa na wajumbe ambao ni Juma Pinto, Michael Wambura, Iman Madega, Salum Abdallah na Isaac Chanji.
Aidha Kamati hiyo imepewa jukumu la kuwashirikisha wadau mbalimbali wampira wa miguu katika kutekeleza majukumu hayo.Wadauwa mpira wa miguu ambao kamati itashirikiana nao ili wajumuike na kusaidia majukumu mbalimbali katika kamati hiyo wanaombwa waitikie wito huo.
Mungu ibariki Taifa Stars,
Mungu ibariki Tanzania.
Chanzo: Tovuti ya TFF