TFF yabainisha mipango yake kuiwezesha Taifa Stars kufanya vizuri kuelekea Kombe la Dunia 2018

Joined
Mar 2, 2012
Posts
57
Reaction score
17

Katika kuimarisha maandalizi ya Timu ya Taifa (Taifa Stars) kuelekea katika mashindano mbalimbali ikiwemo mechi mbili za ugenini na nyumbani dhidi ya Algeria, Rais wa TFF Jamal Malinzi ameunda kamati maalum itakayoitwa "Kamati ya Taifa Stars" ambayo majukumu yake yatakua ni.

(i)Kuimarisha huduma kwa wachezaji,

(ii)Uhamasishaji na Masoko,

(iii)Kuhamasisha wachezaji,

(iv)Kuandaa na kusimamia mkakati wa Ushindi.

Kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Farough Baghouzah, Teddy Mapunda (Katibu), huku ikiwa na wajumbe ambao ni Juma Pinto, Michael Wambura, Iman Madega, Salum Abdallah na Isaac Chanji.

Aidha Kamati hiyo imepewa jukumu la kuwashirikisha wadau mbalimbali wampira wa miguu katika kutekeleza majukumu hayo.Wadauwa mpira wa miguu ambao kamati itashirikiana nao ili wajumuike na kusaidia majukumu mbalimbali katika kamati hiyo wanaombwa waitikie wito huo.

Mungu ibariki Taifa Stars,
Mungu ibariki Tanzania.


Chanzo: Tovuti ya TFF
 
Mimi hizi kamati huwa naona ni kama kamati za kupiga pesa maana watu ni walewale na bado tunapighwa tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…