Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeeleza kusikitishwa na taarifa zinazozagaa mitandaoni kuhusu uhalali wa mchezaji Muhamed Ame kuchezea Timu ya Taifa (Taifa Stars).
TFF imefafanua kuwa Ame ni miongoni mwa wachezaji 23 walioorodheshwa rasmi kwa mechi dhidi ya Guinea, na alikaguliwa pamoja na wachezaji wengine na timu pinzani pamoja na Kamishna wa mechi kabla ya kuruhusiwa kucheza.
Pia, Soma: Tanzania hatarini kuondolewa AFCON 2025 baada ya kukiuka kanuni za Shirikisho la Soka la Afrika (CAF)
Mechi hiyo ya mchujo ya AFCON, iliyochezwa jijini Dar es Salaam, ilimalizika kwa ushindi wa 1-0 kwa Taifa Stars, ushindi uliowahakikishia nafasi katika fainali za AFCON 2025.
TFF imeongeza kuwa haina taarifa yoyote rasmi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuhusu madai ya kutokuwa halali kwa ushiriki wa Ame katika mechi hiyo.