TFF yamfungua Kocha Luc Eymael kwa miaka miwili na kumpiga faini ya Tsh. Milioni 8 kutokana na kauli zake za kibaguzi

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), imemfungia miaka miwili na faini ya sh 8 milioni kocha wa Yanga, Luc Eymael.

Eymael ametiwa hatiani kwa makosa mawili ikiwemo ubaguzi na udhalilishaji na tuhuma dhidi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Mjumbe wa kamati ya Nidhamu ya TFF, Alex Mushumbusi amesema wameridhika na ushahidi uliotolewa dhidi ya kocha huyo na atanza kutumikia adhabu hiyo kuanzia leo.

Hata hivyo Mushimbuzi amesema Eymael ana haki ya kukata rufaa katika ngazi ya juu ambayo ni Kamati ya Rufaa ya TFF.

Eymael anatuhumiwa kufanya kosa hilo baada ya mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli ambapo Yanga ilishinda bao 1-0, mechi iliyochezwa Uwanja wa Samora mkoani Iringa.

Hata hivyo, Yanga baada ya kumfuta kazi, TFF walitoa taarifa ya kumchukulia hatua kali za kinidhamu kocha huyo huku Cham cha Soka Afrika Kusini (SAFA) nao wakitoa taarifa ya kumfungia kocha huyo kujihusisha na mpira wa miguu nchini humo.

Eymael tayari ameshaondoka nchini na alisema mwanasheria wake atashughulikia masuala yote yanayomuhusu.
 
Alitoa kauli gani? tujuzane wakuu tupate vya kuchangia tunadanganyana sana kwenye kahawa
 
Mashauri kibao wameyakalia la Morison hadi leo hawalitolea maamuzi , la Kabwili hadi leo halijatolewa maamuzi, yule refa wa Kagera na yanga mpaka leo hawajamtolea maamuzi hili kwa sababu adhabu yake imeambatana na pesa wamelitolea maamuzi haraka
 
Mashauri kibao wameyakalia la Morison hadi leo hawalitolea maamuzi , la Kabwili hadi leo halijatolewa maamuzi, yule refa wa Kagera na yanga mpaka leo hawajamtolea maamuzi hili kwa sababu adhabu yake imeambatana na pesa wamelitolea maamuzi haraka
Tulia nyan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…