TFF yamtupia virago kocha wa Taifa Stars!

TFF yamtupia virago kocha wa Taifa Stars!

Source07

Senior Member
Joined
Oct 5, 2018
Posts
196
Reaction score
353
Taarifa za kuaminika zinasema kua kufatia matokeo mabaya walio yapata Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars katika Fainali za Afcon,zimetosha kua sababu za kumfuta kazi kocha Emmanuel Ammunike..Sababu zingine zakumfuta kazi kocha huyo zikiwa nikutafuta kocha atakae weza kuifanya Stars kuweza kufanya vizuri katka michuano ya CHAN inayotarajiwa kuanza baada ya kumalizika kwa Afcon huku hatua za Awali za kufuzu michuano hiyo inayojumuisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya Africa, Stars ikipangwa kuminyana tena na Kenya, Harambee Stars!
Mpaka sasa Tff bado hawajaweka wazi ni nani amekabidhiwa timu mpaka pale kocha mkuu atakapo patikana!
Ammunike is Out!je hiyo ni solution kwa matokeo mabovu kwa Stars?kwenu wanamichezo!
 
Kama taarifa yako ni ya kweli basi TFF watakua wamefanya jambo la msingi. Wangemchukua yule wa Uganda aliyebwaga manyanga ingekua vyema pia. Kiukweli falsafa za Amunike kwa kiasi kikubwa zilikua ni pasua kichwa.
 
Wakutupiwa virago ni mwakyembe na shonza pamoja na rais wa tff huyo amunike anaonewa tu yeye kakuta wachezaji wa mafungu wasio na skill wala ability

Huu ni uzembe wa tff wa kujifungia ofisin badala ya kwenda mikoan kutafuta vipaji

Shonza anakaa tu wizaran akisubili diamond atoe nyimbo aifungie

Upuuz kabisa
 
Tatizo ni pale tunapolenga kufuzu ushiriki wa mashindano na si kutwaa ubingwa wa mashindano. Lakini shida zaidi kutokuwepo sports academies kwa ajili ya vijana kulelewa kimichezo na kama academies ni ngumu kwetu vipi kuhusu vipindi vya michezo mashule navyo tumeshindwa kuvisimamia kwa malengo ya kuimarisha michezo nchini...!!

Na mtazamo wa viongozi wetu wa kisiasa bado haujagundua kuwa michezo ni ajira madhubuti hivyo ipewe kipaumbele kama sehemu muhimu ya malezi na makuzi ya vijana wetu ambao kesho keshokutwa wanaweza kuliletea heshima taifa letu. Tumepuuzia michezo mashuleni na kukazania mifumo dhaifu ya elimu ambayo hata haiwasaidii vijana kupata vipato wamalizapo elimu zao. Amunike sio shida kabisa, shida ni sisi kutokubali kuwekeza kwa kujipa muda wa mafanikio.
 
Mimi ninaweza kujitolea kuinoa Stars kwa mwaka mmoja bila malipo yoyote. Masharti yangu makubwa yatakuwa matatu tu: (a) mkataba wangu wa kufanya kazi hiyo usivunjwe kabla haujaisha, (b) katika kazi yangu ya kuinoa Stars, iwe ni marufuku kwa mtu mwingine yeyote kuingilia utendaji kazi wangu. (c) Ubingwa wa CHAN tutakaochukua mwakani ujulikane nchini kama "Ubingwa wa CHAN kwa Hisani ya Kichuguu"
 
Taarifa za kuaminika zinasema kua kufatia matokeo mabaya walio yapata Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars katika Fainali za Afcon,zimetosha kua sababu za kumfuta kazi kocha Emmanuel Ammunike..Sababu zingine zakumfuta kazi kocha huyo zikiwa nikutafuta kocha atakae weza kuifanya Stars kuweza kufanya vizuri katka michuano ya CHAN inayotarajiwa kuanza baada ya kumalizika kwa Afcon huku hatua za Awali za kufuzu michuano hiyo inayojumuisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya Africa, Stars ikipangwa kuminyana tena na Kenya, Harambee Stars!
Mpaka sasa Tff bado hawajaweka wazi ni nani amekabidhiwa timu mpaka pale kocha mkuu atakapo patikana!
Ammunike is Out!je hiyo ni solution kwa matokeo mabovu kwa Stars?kwenu wanamichezo!
Wamchukue Bongo Zozo kama wamekosa kocha
FB_IMG_1562527268321.jpeg
FB_IMG_1562527315988.jpeg
 
Taarifa za kuaminika zinasema kua kufatia matokeo mabaya walio yapata Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars katika Fainali za Afcon,zimetosha kua sababu za kumfuta kazi kocha Emmanuel Ammunike..Sababu zingine zakumfuta kazi kocha huyo zikiwa nikutafuta kocha atakae weza kuifanya Stars kuweza kufanya vizuri katka michuano ya CHAN inayotarajiwa kuanza baada ya kumalizika kwa Afcon huku hatua za Awali za kufuzu michuano hiyo inayojumuisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya Africa, Stars ikipangwa kuminyana tena na Kenya, Harambee Stars!
Mpaka sasa Tff bado hawajaweka wazi ni nani amekabidhiwa timu mpaka pale kocha mkuu atakapo patikana!
Ammunike is Out!je hiyo ni solution kwa matokeo mabovu kwa Stars?kwenu wanamichezo!
Rais wa TFF anapaswa kujiuzulu kwa kuendesha TFF kama vile ni Bavicha au UVCCM!
 
misri kaanza kujiuzulu rais wa chama chao cha soka... akafata kocha...

bongo msala anauziwa kocha.. huku tff wanakomaa kula hela za bure tu..

rais wa tff alipaswa asepe fasta
 
Kwa wenzetu Misri baada ya kichapo cha jana kocha, rais wa shirikisho Nchini misri pamoja bodi nzima wamebwaga majanga..
Nilitegemea na bongo iwe hivyo
 
Kocha mpya apige marufuku wenyeviti wa the so called "kamati za kuhamasisha ushindi" kujisogeza kwenye timu na kusambaza mikosi na mabalaa yao
 
misri kaanza kujiuzulu rais wa chama chao cha soka... akafata kocha...bongo msala anauziwa kocha.. huku tff wanula hela za bure
Rais wa chama alimtimua kwanza kocha harafu na yeye ndio akaresign. Kasema ni moral obligation. Huku kwenu hiyo misamiati huwa haipo
 
Taarifa za kuaminika zinasema kua kufatia matokeo mabaya walio yapata Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars katika Fainali za Afcon,
Ni matokeo gani mazuri tulikuwa tunatarajia mpaka haya tuite mabaya?
 
Rais wa TFF anapaswa kujiuzulu kwa kuendesha TFF kama vile ni Bavicha au UVCCM!
Na huu ndio ungekuwa uwamuzi sahihi, kila mtu awajibike kwa nafasi yake. Kocha ni matokeo ya timu na mifumo dhaifu.
 
Nikianza kwenu nyie na huyo kalia sijui kakaria! na hiyo tifuatifua!
walitaka tuchukue kombe na timu ile tulioenda nayo??? kweli??
Amunike kwanza kajitahidi sana team ina makosa mengi, mapungufu ya kushato halafu hiyo CHAN aje kocha mwingine tuanze upyaaa!🤑🤑😠😠

Shenzy kabisa hiyo tifuatifua
 
Back
Top Bottom