TFF Yapokea maombi ya Kagame CUP 2015

TFF Yapokea maombi ya Kagame CUP 2015

Dotto Mnzava

R I P
Joined
Mar 6, 2014
Posts
864
Reaction score
427
Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini TF, leo hii limepokea maombi toka Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), likiitaka Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ngazi ya vilabu yatakayotimua vumbi kuanzia mwezi Julai mwaka huu.

Kufuatia maombi hayo ya uenyeji wa michuano ya CECAFA kwa ngazi za vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame CUP), TFF inatafakari juu ya maombi hayo na itayatolea maamuzi.

SEMINA YA MAKOCHA WAKUFUNZI

Semina ya Makocha wakufunzi inatarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam kuanzia Aprili 27, 2015 na kumalizika Mei 2 Mwaka huu ikiwajumuisha jumla ya makocha wakufunzi 21.

Watakaohudhuria semina hiyo na leseni zao kwenye mabano ni; Michael Bundala (A) Ilala, Leodgar Tenga (A) Kinondoni, George Komba (A) Dodoma, Don Korosso (A) Kyela-Mbeya, Wilfred Kidao (B) Ilala, Rogasian Kaijage (A) Mwanza, Mkisi Samson (B) Mbeya, Dr. Mshindo Msolla (A) Kinondoni, Ally Mtumwa (A) Arusha, Madaraka Bendera (A) Arusha.

Wengine ni Juma Nsanya (A) Tabora, Hamim Mawazo (A) Mtwara, Wanne Mkisi (B) Kinondoni, Major Abdul Mingange (A) Kinondoni, Dr. Jonas Tiboroha (C) Ilala, Nasra Mohamed (A) Zanzibar, John Simkoko (B) Morogoro, Juma Mgunda (B) Tanga, Triphonia Temba (B) Manyara, Ambonisye Florence (C) Pwani, na Eugen Mwasamaki (B) Dar es salaam.

VPL KUENDELEA KESHO

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea kesho jumanne kwa mchezo mmoja katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, vinara wa ligi hiyo Young Africans watawakaribisha timu ya Stand United kutoka mjini Shinyanga.

Ligi hiyo itaendelea siku ya jumatano kwa michezo miwili, Simba SC watakuwa wenyeji wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Polisi Morogoro wakiwakaribisha Coastal Union katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Imetolewa na Shirikisho la Mpira wa MiguuTtanzania (TFF)
 
Hayo mashindano yakipita,simba itakaa majukwaani wakishuudia wanaojua mpira azam,yanga na mbeya wakikipiga
 
Kagame CUP..ndani ya Azam TV rahaaa sana!!
 
Hayo mashindano yakipita,simba itakaa majukwaani wakishuudia wanaonua mpira azam,yanga na mbeya wakikipiga
wapi lazima Musonyeatalazimisha Simba ishiriki ili wavute mpunga na TFF wakilazimisha washiriki Mbeya CITY atasema kuwa wanamuhujumu
 
kama mashindano hayo ya bonanza kagame cup yatafanyika hapa TZ. viongozi tunawaomba msishiriki kama mtashiriki ni sawa na watumwa musonye kawatukana sana yanga kawadharirisha kawafedhuri aidha musonye aombe radhi wanayanga kupitia vyombo vya habari kama alivyowatukana.
kwa timu inayoshiriki cecafa humpa mwenyekiti asante ya shs milioni mbili mpaka tatu viongozi mkikurupuka mkashiriki tutajua mmepokea rushwa kutoka cecafa
 
kama mashindano hayo ya bonanza kagame cup viongozi tunawaomba msishiriki kama mtashiriki ni sawa na watumwa musonye kawatukana sana yanga kawadharirisha kawafedhuri aidha musonye aombe radhi wanayanga kupitia vyombo vya habari kama alivyowatukana.
kwa timu inayoshiriki cecafa humpa mwenyekiti asante ya shs milioni mbili mpaka tatu viongozi mkikurupuka mkashiriki tutajua mmepokea rushwa kutoka cecafa

Ha ha ha haaaaaa jina lako limenivutia sana, ikiwezeka naomba tubadilishane mkuu...
 
ni muda muafaka sasa TFF kulinda heshima yetu musonyi ni mtu mwenye dharau aliyoyoyafanya yalikua dharau kwa nchi hii malinzi kataa hiyo ofa waende hukohuko mashindano yafanyike hapa endapo huyo mwenye dharau atakapo achia nafasi hiyo ameharibu mashindano kwakujifanya mjuaji sasa ni muda tanzania kushika nafasi hiyo muhimu
 
kama mashindano hayo ya bonanza kagame cup viongozi tunawaomba msishiriki kama mtashiriki ni sawa na watumwa musonye kawatukana sana yanga kawadharirisha kawafedhuri aidha musonye aombe radhi wanayanga kupitia vyombo vya habari kama alivyowatukana.
kwa timu inayoshiriki cecafa humpa mwenyekiti asante ya shs milioni mbili mpaka tatu viongozi mkikurupuka mkashiriki tutajua mmepokea rushwa kutoka cecafa

nimekuelewa sana nchi hii ndio maana tunadharauliwa sana tunashindwa kutunza heshima kama nchi ni upuuzi mtu anaonesha dharau na matusi kwa taifa letu leo anakuja tena anafata nini malinzi tulindie heshima yetu na nyinyi waandishi wa muichezo chama chenu kitumieni hili lisifanikiwe
 
Hayo mashindano yakipita,simba itakaa majukwaani wakishuudia wanaojua mpira azam,yanga na mbeya wakikipiga

Vipi Mkuu yahoo hatimaye umefufuka! Hali ilikiwaje huko 'pulgatory'? Karibu sana, achana na mashabiki wa mikia wenye dalili za kukulengesha kwenye ban tena.

TFF isikubali ombi la Musonye, wamwambie black and white kuwa Tanzania haiwezi kuandaa mashindano hayo hadi atakapoachia ngazi pale CECAFA.

CC. Jamal Malinzi: Kwa hatua zako muhimu.
 
Last edited by a moderator:

Asnte mkuu yule jamaa sijui alitumwa na aveva....anyways nilikuwa nasikia maombi yako ya rip nilipokuwa akhera .... na yamenisaidia kusamehewa zambi zangu
 
Last edited by a moderator:
Hii dunia ya CECAFA ya ajabu sana. Miezi mitatu kabla mashindano ndio wanateua nchi ya kuandaa?
Hawana calendar hata ya miaka miwili mbele ?

TFF wasikubali upuuzi huu. Labda mwakani na zishiriki club Bingwa za nchi tu. Kuingiza timu za mchangani ndio kuwaua mashindano haya .

Imefika mahali CECAFA wawe na calendar. Sidhani kama COSAFA wanaenda kwa kubahatisha namana hii. Tenga mwondoe Musonye CECAFA isonge mbele vinginevyo itakufia mikononi mwako!
 
nimekuelewa sana nchi hii ndio maana tunadharauliwa sana tunashindwa kutunza heshima kama nchi ni upuuzi mtu anaonesha dharau na matusi kwa taifa letu leo anakuja tena anafata nini malinzi tulindie heshima yetu na nyinyi waandishi wa muichezo chama chenu kitumieni hili lisifanikiwe

aaha mkuu waandishi kwa hilo bonanza nawasiwasi wanapata posho maana naona wameshangilia sana dawa serikali ikatae sababu kuna uchaguzi na kupigia kura katiba pendekezwa
 
Hii dunia ya CECAFA ya ajabu sana. Miezi mitatu kabla mashindano ndio wanateua nchi ya kuandaa?
Hawana calendar hata ya miaka miwili mbele ?

TFF wasikubali upuuzi huu. Labda mwakani na zishiriki club Bingwa za nchi tu. Kuingiza timu za mchangani ndio kuwaua mashindano haya .

Imefika mahali CECAFA wawe na calendar. Sidhani kama COSAFA wanaenda kwa kubahatisha namana hii. Tenga mwondoe Musonye CECAFA isonge mbele vinginevyo itakufia mikononi mwako!
CECAFA kama TFF tu, hawana jipya! Kwanin huyo musonye habanduki hapo cecafa au ana hisa za kwenye hilo shirikisho la vyama vya mpira wa miguu kwa nchi za Afrika mashariki na kati?!
Subir kwanza tuone madudu yao.........
 
Back
Top Bottom