TFF yaunda Kamati ya ushauri ya Ligi

Dotto Mnzava

R I P
Joined
Mar 6, 2014
Posts
864
Reaction score
427
Rais wa Shirikiso la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Jamal Malinzi ameteua Kamati ya ushauri ya Ligi Kuu (VPL) na ligi Daraja la Kwanza (FDL) nchini.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ni Alhaj Ahmed Mgoyi na katibu wa Kamati ni mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi nchini (TPLB) na wajumbe wengine saba.

1. Alhaji Ahmed Idd Mgoyi (Mwenyekiti)
2. Boniface Wambura (Katibu)
3. Kennedy Mwaisabula- Mjumbe
4. Idd Mshangama- Mjumbe
5. Amiri Mhando- Mjumbe
6. Grace Hoka- Mjumbe
7. Ibrahim Kaude (Vodacom)- Mjumbe
8. Baruan Muhuza (Azam Media)- Mjumbe
9. Peter Simon- Mjumbe

Kazi za kamati hiyo zitakua ni:
(i) Kufuatilia mwenendo wa Ligi
(ii) Kuishauri Bodi/TFF namna ya kuboresha Ligi
(iii) Masoko
(iv) Leseni za Vilabu (Club Licensing)
(v) Mipango ya Maendeleo ya Vilabu
(vi) Viwanja vya mazoezi
(vii) Utoaji wa tuzo za ligi mbalimbali
(viii) Kutengeneza vigezo (criteria) vya washindi wa tuzo



IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
 
Hizi kamati zote za TFF zina msaada gani wa maendeleo ya mchezo wa soka nchini?
 
Mbona magufuli simuoni kwenye orodha? Au wamemkata?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…