TFF yawaita Simba, Singano Juni 9

TFF yawaita Simba, Singano Juni 9

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,229
Reaction score
610
TFF imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mgogoro wa kimkataba kati ya Mchezaji Ramadhani Singano na klabu ya Simba.

TFF imeagiza mwakilishi wa klabu ya Simba pamoja na mchezaji wa Ramadhani Singano wafike ofisi za TFF siku ya Jumanne tarehe 09/06/2015 kwa mazungumzo.

Kila upande umetakiwa uje na vielelezo vyake.

Katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mazungumzo,TFF inaziasa pande zote mbili zijiepushe na kutoa matamko yanayoweza kuchochea hali ya kutoelewana na kuamsha hisia mbaya katika familia ya mpira wa Miguu Tanzania.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Best Regards,
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
 
Duh soka ya bongo,kudadadeki. Yaani si tunasubiri mtuambie mkataba uliokuwa kwenu unasemaje nyie mnaita watu kwa mazungumzo kweli hii tifuatifua
 
Aisee maskini kijana huyu na elimu yake ya kuunga unga natoa wito kwa wanajamii forum hasa wale waliosomea mambo ya sheria wamsaidie huyu kijana msikubali aende peke yake siku hiyo unategemea nini kulia kakaa malinzi kushoto aveva. Ilo bit atakalopigwa ataishia kusaini mkataba mwingine wa miaka miwili kwa mshahara wa laki tano arafu tuje kuambiwa TFF imewasuruhishwa na aonekane yeye ndiye akusoma vizuri mkataba. Nimeoneshwa makazi anayoishi kupitia globu moja hivi aisee hana tofauti na maisha ya mama ntilie.. naomba wanajamiiforums tutumie nafasi hii kumsaidia hizi klabu zimekuwa na na kamchezo haka unasainishwa mkataba arafu badae last page inachakachaliwa kwenye mkataba mwingine magumashi.
 
kwanza aliambiwa atalipiwa nyumba hajalipiwa kama tff kweli tff imsaidie huyo kijana kama itakuwa itahongwa ikamuumiza singano tutaita TANZANIA FITINA FEDARATION (TFF)
 
Hahahahaha
 
Aisee maskini kijana huyu na elimu yake ya kuunga unga natoa wito kwa wanajamii forum hasa wale waliosomea mambo ya sheria wamsaidie huyu kijana msikubali aende peke yake siku hiyo unategemea nini kulia kakaa malinzi kushoto aveva. Ilo bit atakalopigwa ataishia kusaini mkataba mwingine wa miaka miwili kwa mshahara wa laki tano arafu tuje kuambiwa TFF imewasuruhishwa na aonekane yeye ndiye akusoma vizuri mkataba. Nimeoneshwa makazi anayoishi kupitia globu moja hivi aisee hana tofauti na maisha ya mama ntilie.. naomba wanajamiiforums tutumie nafasi hii kumsaidia hizi klabu zimekuwa na na kamchezo haka unasainishwa mkataba arafu badae last page inachakachaliwa kwenye mkataba mwingine magumashi.
Nami nimesoma kwenye blog ya shaffih Dauda nimeshangazwa sana,ambapo walim wake wamewakana kabisa viongozi wa SIMBA,ila pia stori ya kughushi Contract nayo inachanganya sana,maana hata huo mkataba wa Singano uliopo TIFUTIFU unaonesha ni wa miaka mitatu wakat dogo ana wa miaka miwili,uhuni kwenye soka unalelewa na haohao TIFUTIFU wa Mchikichini kwa Jamal Malinzi ila hapo kwenye green let me believe kuwa hujakosea
 
Last edited by a moderator:
Sorry I meant blog... Mwenye number yake ya simu aweke hapa plse tumuamshe asijekuwa anajihami na mkataba wake akishapigwa AC ya TFF atachanganyikiwa
 
Duh soka ya bongo,kudadadeki. Yaani si tunasubiri mtuambie mkataba uliokuwa kwenu unasemaje nyie mnaita watu kwa mazungumzo kweli hii tifuatifua

Na mimi nilitegemea hivyo mkuu, sijui nini kinafichwa fichwa hapo
 
PAMOJA KWAMBA MIMI NI MWANA SIMBA..ILA NIMECHUKIZWA NA HUU UPUUZI NA UNYONYAJI..yaani dogo anavyopiga mpila vile,kumbe ana maisha magumu..nchi hii mafisadi kila kona
 
Nami nimesoma kwenye blog ya shaffih Dauda nimeshangazwa sana,ambapo walim wake wamewakana kabisa viongozi wa SIMBA,ila pia stori ya kughushi Contract nayo inachanganya sana,maana hata huo mkataba wa Singano uliopo TIFUTIFU unaonesha ni wa miaka mitatu wakat dogo ana wa miaka miwili,uhuni kwenye soka unalelewa na haohao TIFUTIFU wa Mchikichini kwa Jamal Malinzi ila hapo kwenye green let me believe kuwa hujakosea

Ya Athuman Idd Chuji yamkuta Singano. Mambo ya Simba hayo. Nakumbuka suala la Chuji lililazimika kuchunguzwa na polisi chini ya Tibaigana. Mwisho wa siku lilimalizwa kisiasa ili kulinda hadhi za wakubwa!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom