TFF yazindua jezi mpya za Taifa Stars

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetambulisha jezi mpya zitakazotumiwa na Taifa Stars ikiwemo jezi ya nyumbani, jezi ya ugenini na jezi namba tatu.

Oktoba 11, 2020 Tanzania itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi, jijini Dar es Salaam ambapo tayari Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amewasili nchini jana kwa ajili ya maandalizi.

Aidha, Kampuni ya Bia ya Serengeti Premium Lager imeingia makubaliano na kusaini mkataba wa Tsh. Bilioni 3 na TFF wa kuidhamini Taifa Stars kwa kipindi kingine cha miaka 3.


View attachment 1592083
 
Ukiondoa nembo ya TFF, sioni jezi ya kitaifa hapo
 
Yanga ni timu ya Wananchi wa Tanzania na timu ya Taifa nayo ni ya Wananchi wa Tanzania!
Simba ni timu ya wenye nchi. Haya wananchi kapangeni foleni kupiga kura kutuchagua wenye nchi, tuwapangie mambo ya kufanya na kutofanya
 
Ni nzuri ila kwanini huwa wanalazimisha rangi zote za kwenye bendera ziwepo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…