Huu mkataba umevunja kanuni ya "conflict of interest" ndio maana TFF wanahangaika kuwazuia watu wasihoji, huu udikteta umepitwa na wakati, huo mkataba lazima uhojiwe.
Haiwezekani mdhamini mmoja avidhamini vilabu vitatu tofauti kwenye ligi moja, hapa uwezekano wa kupanga matokeo ni mkubwa sana, na zaidi, mdhamini huyo huyo bado nae anaidhamini ligi, kwa hawa waamuzi wetu walivyo wa hovyo uwezekano wakuipendelea/kuzipendelea klabu za mdhamini ambae ndie bosi wao ni mkubwa sana.
Naamini pesa za kuwalipa hawa waamuzi hutoka kwa wadhamini kupitia TFF, hili lazima lizungumzwe vizuri na TFF wasilete ubabe wa kishamba kwenye hili.
Ni kichekesho mkataba wa udhamini unaovihusu vilabu vyote shiriki vya ligi kuu usijadiliwe na vilabu husika, huu ni ujinga wa hali ya juu sana na aibu kwa uongozi wa TFF.
Vilabu shiriki vina haki ya kuhoji chochote kilichopo ndani ya huo mkataba kwasababu ni wahusika, kama TFF na GSM hawataki, basi GSM ajitoe kuvidhamini vilabu vingine, vibaki hivyo vitatu tu, [Yanga, Namungo, na Coastal Union] na GSM wajitoe kuidhamini ligi kuu.
Huu ni uthibitisho mwingine mpira wa Tanzania una matatizo kuanzia juu kabisa kwenye uongozi, mambo kama haya yanayojitokeza ni aibu kwa mpira wetu na nchi yetu.