Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Nilikuwa shambani nalima jioni ya Alhamisi karibu na kisiwa cha Belle Isle nje ya Jiji la Detroit. Mara nikasikia sauti iliyoniita na kusema ‘Mwanakijiji!' nikaitika ‘Naam!". Ikaniambia "Sogea hapa". Basi pole pole nikaelekea iliko sauti hiyo. Nilipokaribia ikaniamuru nisimame na nisiendelee mbele zaidi. Nikaona upande wa kushoto kwangu kichaka kikiwaka moto; kichaka kile kilikuwa kinateketea taratibu na matawi yake kugeuka makaa na majivu. Chini ya Kichaka kile pameandikwa Tanzania. Nikaogopa na kutetemeka. Sauti ile ikaniamuru "Usiogope! Vaa Viatu vyako, maana hapo unaposimama pana ufisadi".
Basi nikafanya hima kuvaa viatu vyangu na kukusanya matambara yangu ya shambani nikisubiri agizo jingine. Sauti ile ikaniambia "Tazama nakupa amri zangu, amri ambazo utawapelekea wana wa Tanzania ili wazishike na kuzifuata." Mara sauti kama ya ngurumo ya radi ikasikika na mwanga mkali kutoka angani ukaangaza na kunipofusha macho yangu. Nilipoyafungua nilijikuta nimevaa miwani myeusi ya jua na mbele yangu kuna laptop iliyoshikwa na mikono ya mtu asiyeonekana.
Nikaona na tazama, maandishi makubwa ya mtindo wa "Old German" yakatokea na sauti ikasema: " Zishike moyoni na uwapelekee Watanzania amri hizi!". Hizi ndiyo amri 10 za serikali ya Tanzania
Amri ya Kwanza: Mimi ndiyo serikali yenu ya Chama Cha Mapinduzi, hakuna serikali nyingine.
Amri ya Pili: Usilitaje bure jina la serikali yako ya Chama cha Mapinduzi, hasa kama wewe ni mpinzani au hauna chama. Kuitaja taja serikali kwa kila tatizo kutakuletea matatizo kwani serikali hii humfuatilia mtu na familia yake hadi kizazi cha nne cha Wanaopandikiza mbegu za chuki. Kama huamini waulize kina Kambona.
Amri ya Tatu: Ishike na kuikumbuka siku ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi, ukiisahau Chama kitakukumbusha kila ifikapo Februari.
Amri ya Nne: Waheshimu viongozi wa Chama cha Mapinduzi na serikali yake pamoja na watoto wa watoto wao ili upate mafanikio katika biashara zako na siku zako za kunufaika na ufisadi ziongezeke.
Amri ya Tano: Usinikosoe
Amri ya Sita: Usiibe mali za CCM
Amri ya Saba: Usiseme nasema Uongo.
Amri ya Nane: Usizitamani sera ambazo si zako wala mali zozote za CCM.
Amri ya Tisa: Usiwashuhudie watu juu ya udhaifu wa viongozi wao na kuwafumbua macho juu yangu.
Amri ya Kumi: Usisimame kutetea mali za nchi yako na wala usiwe na kimbelembele cha kujifanya wewe ni mwanaharakati wa mabadiliko. Nitakumaliza.
Ndipo miguu yangu ikanyong'onyea kwa hofu. Ndipo sauti ile ikaniagiza kupeleka ujumbe wa Unabii wake kwa njia ya makala. "Ninakutuma uwaandikie maneno nitakayokupa kwani wakati umefika wananchi wasikie NENO kutoka kwa serikali yao!" Akanipa maneno ambayo nimeyaweka moyoni hadi wiki ijayo kwenye mojawapo ya makala zangu. Yatakuwa ni maneno ambayo yatawatikisa watawala na yatawashtua watawaliwa.
Kuna wazee niliowaacha kilabuni wakati naenda shamba; waliponiona narudi huku uso unatabasamu wakaambiana "huyu naye amesikia sauti". Wakasema "Amen Amen" huku wakiendelea kupokezana kombe la mbege. Kwa mbali wimbo wa "umkombhoti" wa Yvonne Chakachaka ukisikika kwa mbali.