Tha PLATINUMZ family show

Mimi naona kama nchi waruhusu tu utoaji mimba, uvutaji bange na homosexuality Kwasababu watu wanafanya na kutangaza pia wanafanya.

Sasa kama hawakamatwi na kuhojiwa maana yake ni halali.

Hatuwezi kuwa na sheria zenye MACHO.

Na kuhusu masuala ya Show, labda nikwambie siyo kila "niche" inaweza kuwa monetized.

Unaweza kufungua website ya ngono ukapata lundo la watembeleaji lakini usipate hata 100.
 
Project write up inaweza kuangalia upande wa biashara zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Mama Diamond anasema kuwa, mzee Abdul hakuwa baba mzazi wa Diamond, inakuaje tena (yeye huyo huyo) aseme kwamba, mzee Abdul aliikataa mimba? Alikataaje kitu (mimba) ambacho si chake? Na kama ni kweli ALIIKATAA, maana yake ni kwamba, basi mama Diamond alitaka kumpa hiyo mimba.
Kwanini alitaka kumpa kitu (mimba) ambacho siyo chake? Kwa lugha rahisi alitaka KUMBAMBIKIA). Je, kosa la mzee Abdul ni kukataa kubambikwa?

2. Mama Diamond amesema kwamba, mzee Abdul hakuwa baba mzazi wa Diamondβ€”alikuwa ni baba mlezi tu. Pia, yeye huyo huyo akasema tena kuwa, mzee Abdul aliahidi kumlea Diamond lakini HAKUMLEA (rudia hilo nenoβ€”HAKUMLEA). Na hata yeye (mama Diamond) hakuwahi kuishi kwa mzee Abdulβ€”na hata picha walizoonekana wakiwa pamoja (kipindi Diamond akiwa mtoto), ilikuwa tu wamepita kumsalimia mzee Abdul hapo Magomeni alipokuwa akiishi.
Je, mtu ambaye umesema hakuwa baba mzazi wa mtoto, na umesisitiza kuwa HAKUMLEA, hicho cheo cha "BABA MLEZI" kilitoka wapi? Alikuwa analea nini?

3. Mama Diamond amesema, mzee Abdul alikataa mimba (ubaya), lakini pia amesema, hakuwa akihudumia kama alivyoahidi (ubaya), pia amesisitiza kuwa, mimba haikuwa yake (ubaya). Kwa lugha rahisi, mama Diamond ameamua kumpaka UBAYA mzee Abdul.
Kama hayo ni kweli, je, hizo pesa ambazo mama Diamond alikuwa anapewa mara kwa mara na Diamond ili akampatie mzee Abdul zilikuwa zinakwenda kwa mzee Abdul kama nani? (Maana mtoto hakumzaa yeye, na wala hakumlea).

4. Mama Diamond amesema, alimpa Diamond ubini wa Abdul kwa sababu (mzee) Abdul ndiye aliyempeleka hospitali kujifungua. Pamoja na hayo, amesisitiza kuwa bwana Salum Nyange (anayemtaja kuwa ndiye baba mzazi wa Diamond), alikuwa anakwenda Tandale kumangalia mtoto (Diamond) kama kawaida. Maana yake ni kwamba, mzee Salum Nyange hakumkataa mtoto. Swali: Inawezekanaje mtu yule yule (mzee Abdul) aliyetaka kubambikwa mimba akaikataa, ndiye akasimama kidete kumpeleka mama Diamond hospitali?
Kama mwenye mimba (Salum Nyange) alikuwepo na hakukataa mimba, ilikuwaje mama Diamond ampe mtoto (Diamond) u-bini wa mtu mwingine (mzee Abdul) kisa tu alimpeleka hospitali kujifungua? Je, ilikuwaje mzee Abdul akaahidi KUMLEA Diamond ilhali baba mzazi wa Diamond (bwana Salum Nyange) alikuwa hai na alikuwa anakwenda kumwangalia mtoto?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili sakata chanzo cha mvurugano ni mama dangote, yani unakuja kuropoka sahivi yote haya, alikua wapi siku zote hizo kuweka ukweli bayana sahivi nikumpa mzee wa watu stress na kumdhalilisha kwa umma especially kipindi hichi mtoto wao Diamond ni maarufu, kwa kweli mjifunze kuishi na wanawake kwa akili sana ni watu hubadilika hubadilika kwa maslahi yao binafsi na sio maslahi yenu ya pamoja
 

Akijibu haya maswali mnitag.
 
Kama Mimba sio ya mzee Abdul kwanini Mama Diamond aseme mzee alikataa mimba?


Kama mzee Abdul sio baba wa Diamond kwanini Mama Diamond alalamike Mzee Abdul kutokumtunza Diamond ? Kwanini hizo lawama asizitupie kwa Baba Diamond?


Kwanini lawama za kutomlea Diamond zielekezwe kwa Baba mlezi na sio Baba mzazi mzee Nyange ambae alifariki mwaka 2004 diamond akiwa ameshakuwa mkubwa ?
 
Labda ndio game lenyewe limeanza.
Fursa ni pesa kaka, si unaona tunavyotumia bandos kuona/kusikiliza simulizi zao,achilia mbali ajira kwa waandishi wa habari za mitandao, magazeti nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…