Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Maelfu ya waandamanaji wakiwa na magari na baiskeli walikusanyika leo kwenye mji mkuu wa Thailand, Bangkok kumtaka waziri mkuu Prayut Chan-O-Cha kujizulu kutokana na jinsi alivyolishughulikia jana la virusi vya corona.
Waandamanaji hao wamejitokeza kwa wingi na kufanya mikusanyiko mikubwa mitatu katikati ya mji ikiwa ni sehemu ya maandamano yanayoendelea nchi nzima dhidi ya serikali ya Cha-O-Cha.
Taifa hilo la kifalme linakabiliwa na wimbi baya kabisa la maambukizi ya virusi vya corona yanayosababisha vifo na kuzidiwa kwa mfumo wa kutoa huduma za afya.
Hasira imeongezeka baada ya kusuasua kwa kampeni ya utoaji chanjo iliyolazimisha serikali kuamuru kuendelea kufungwa kwa shughuli nyingi za biashara zinazotegemewa na raia wa taifa hilo.
Hadi sasa zaidi ya watu laki 9 wameambukizwa virusi vya corona na 7,751 wengine wamepoteza maisha.