Thamani ya mtu huonekana pindi anapotoka katika mzunguko wako wa maisha

Thamani ya mtu huonekana pindi anapotoka katika mzunguko wako wa maisha

Joined
Jul 27, 2022
Posts
94
Reaction score
134
Kuna namna nyingi binadamu wa sasa tunazitumia kuonesha thamani ya mtu.

Wengine tunamthamini mtu pindi tu tunapokuwa na uhitaji yaaani anakuwa na thamani pindi anaponipa huduma fulani ila ikiisha tu na thamani yake pia inapungua, inaisha ama inapotea kabisa.

Kuna Wengine tunawathamini kwa vipindi, yaaani wana thamani kwenye shida ama tunapohitaji michango yao kwenye shughuli zetu mbalimbali.

Ila tukumbushane tu ule msemo usemao "Thamani ya mtu huonekana pindi anapotoka katika mzunguko wako wa maisha/kazi" tuutunze uthamani wa kila binadamu tuliyeruhusu aingie katika maisha yetu.

Tuutunze uthamani kwa kujuliana hali, kutiana moyo, kushauriana na kuwasiliana mara kwa mara inapobidi ili tukikutana na uhitaji wa namna yoyote ile iwe rahisi kushikana mikono.

Hurka ya binadamu ni kukosea, kuna waliosema hata vikombe kabatini hugongana hivyo msamaha uwepo baina yetu ili tuendelee kutunza thamani ya kila mmoja wetu.

NAKUTHAMINI RAFIKI YANGU.
 
Binadamu saiv ni ngumu sana labda enzi ya Utume wa yesu ndio aliweza kudhamini Kila mtu.
 
Kama hauna pesa hutatoswa Hadi na ndugu

Mara nyingi watu wenye pesa wanakuaga na tabia Njema ndo wanaheshimiwa Sana .

Mfana hapa uswahilini watu hawaheshimiki kutokana na tabia zao walizonazo
 
mwalimu Dimitry, aidha uko nyuma ya mda au uko Pluto

ila kwa karne hii, huku Duniani tuliko, huthaminiwi bila Pesa, ipo hivyo huwezi badili
Najaribu tu kutafuta namna tunavyoweza kurejesha yale mazuri yaliyotoweka ndugu yangu kwa kudhani tukibadilika sisi basi tunaweza kubadili vizazi vyetu pia.
Tujaribu rafiki yangu
 
Back
Top Bottom