Thamani ya ukweli hapa nchini

mwamagunda

Member
Joined
Feb 27, 2011
Posts
13
Reaction score
0
Nipo kazini kwa muda mrefu kidogo hivi sasa!
Wakati naanza kazi nilikuwa na matumaini makubwa ya kutoa mchango mkubwa katika utoaji wa huduma katika eneo langu la kazi, lakini naweza kusema hali halisi inanikatisha tamaa, japo bado sijakata tamaa bado!
Katika utumishi wa serikali hivi sasa (angalau mahali fulani) kutosema ukweli hasa pale mambo fulani yakienda mrama! Anayesema ukweli anageoka kuwa adui wa karibu kila mtu, hata wale ambao ni wazi kuwa hawanufaiki kwa lolote na uwongo humshangaa mwenye kusema ukweli!
Tunakwenda wapi?
 
Kuna haja ya watu kuelekezwa maudhui ya kila jukwaa na kujua threads zipi ziende wapi.
B2T: sema ukweli siku zote usiogope watu watakutreat vipi.
 
ukweli ni msumari wa kutu kwa watenda maovu...usiogope kusema ukweli siku zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…