TUKANA UONE
JF-Expert Member
- Jan 3, 2018
- 2,345
- 6,970
Nikiwa shule ya msingi kuna mwalimu mmoja alikuwa anaitwa AGNESS, huyu alikuwa mjaluo kutoka huko mkoani Mara, kiukweli alikuwa mzuri wa sura na umbo, huyu mwalimu sitokuja kumsahau hadi naingia kaburini kwasababu alikuwa kisu kwelikweli, kwa leo ndiyo wanaitwa "PISI KALI".
Huyu mwalimu kuna siku aliletwa pale shuleni na gari aina ya Limoussine na akashushwa kwa madaha, kiukweli wakati huo kabla hata sijabalehe lakini nilikuwa nina ufahamu wa kizuri ni kipi na kibaya ni kipi!.
Miaka hiyo kutembelea Limousine haikuwa kitu rahisi kama mnavyodhani, ilikuwa unaonekana wewe ni tajiri kweli kweli!
Yule mwalimu alikuwa mzuri ajabu na wanaume wenye ukwasi walimsalandia kila mara pale shuleni, yule mwalimu alikuwa anaonekana mara 2 kwa wiki pale shuleni, siku nyingine alikuwa hapatikani, kwa bahati nzuri au mbaya alikuwa mwalimu wetu wa darasa.
Sababu ya yeye kutokuonekana ilikuwa ni wanaume waliokuwa wakimchukua wakishinda naye kwenye starehe.
Alikuwa mzuri sana na kiukweli huwa nikikumbuka namna alivyokuwa, huwa natamani siku zirudi nyuma nitamani kumuona tena😭😭
Daaah!!.
Juzi moja nilikuwa naongea na classmate wa shule ya msingi wa huko mkoani ananiambia huyo mwalimu alifariki kitambo sana kwa ugonjwa wa Upungufu wa kinga mwilini.
Kiukweli nimelia na kusikitika sana namna nikikumbuka alivyokuwa akiniachia madaftari nisahihishe mimi na mwanafunzi mwenzangu Monica ambaye naye ni Marehemu yaaani nabaki kulia tu 😭😭😭😭
Miaka hiyo ya 1993 namna madam Agness alivyokuwa mzuri halafu nimeambia amekufa nabaki najiuliza sana,laiti angeutunza uzuri wake leo angekuwa mtu mkubwa sana, kipindi kile najua alishawishiwa na gari za kifahari pamoja na fedha za wanaume akaingia mkenge kumbe alikuwa anajichimbia kaburi!😭😭😭😭😭.
Mwaka 1994 ulituharika kwako mimi na Monica hapo kwako kusherehekea Siku kuu ya Christmas, ulitupikia tukala nyama ya bata na pilau zuri kisha wewe ukaja kuchukuliwa na gari aina ya pigeout ukaondoka ukalala hatimaye ukaja kesho yake ukinukia marashi mazuri yenye kupendeza,ulitupatia mimi na Monica shilingi 200 ambazo tuligawana kila mmoja shilingi 100 na kiukweli tuliyafurahia maisha sana kwasababu hiyo hela ilikuwa kubwa mno!.
Ooooh Madam Agness I Cry for you & miss u so much,nitakukumbuka daima,umeondoka na uzuri wako!😭😭😭😭😭
THANK YOU MADAM AGNESS TUTAONANA ASUBUHI ILIYO NJEMA.