Eng. Smasher
JF-Expert Member
- Nov 13, 2010
- 745
- 23
Safi sana, Mungu na JF washukuriwe. Ingawa wengine wanafikiri JF ni sehemu ya porojo na siasa, actually kuna faida nyingi sana ktk kila sector na hasa hii muhimu na nyeti ya afya. Ni baada ya kusoma faida za vitu kama asali, nilianza kubwia asali kama mwendawazimu, na you can tell the difference, mafua, kichwa, tumbo (unakunya kwa raha mustarehe bila kutoka mijasho na kuguna kama unatoa mawe) na magonjwa madogo madogo kwishnei. Unalala na kuamka so fresh !! again, big up all JF members...
Ni wachache sana wanaorudi kushukuru!
Engineer, ithink that Social Engineering!
Ni wachache sana wanaorudi kushukuru!
Engineer, ithink that Social Engineering!
Yeah PJ, Engineering sio Solid Mechanics na thermodynamics tu, siku hizi Engineers wako social sana.
INJINIA SMASHA,
unaniudhi sana vile unavyojifananisha na ST. RR kwa kila kitu
Eng. Smasher. Mungu ashukuriwe. Na namuombea huyo nduguyo Mungu ajiinue kwake na amponye kwa uweza wake arudi katika afya njema. Vile vile asiache kumshukuru Muumba maana ndiye muweza yote na kimbilio letu sote.Niliwahi kutoa maada kuhusu dawa ya KIKOHOZI tatizo lililokuwa linamsumbua ndugu yangu!
Rubi alitoa ushuhuda wake mwenyewe na kuanza kuufanyia kazi!!
Kwa kweli MUNGU ametenda miujiza sasa hivi huyu ndugu yangu ameanza kuacha kukohoa bila kutumia dawa zaidi ya KUNYWA MAJI MENGI awezavyo na MATUNDA!!
Ahsante Rubi MUNGU akubariki na wana JF wote!!!
BIG THANKS kwa GREAT THINKERS!!!
Eng. Smasher. Mungu ashukuriwe. Na namuombea huyo nduguyo Mungu ajiinue kwake na amponye kwa uweza wake arudi katika afya njema. Vile vile asiache kumshukuru Muumba maana ndiye muweza yote na kimbilio letu sote.
Ushauri kwa nduguyo ajitahidi sana kuwa makini kwa vyakula na mazingira yanayomzunguka. akiweza kupunguza matumizi ya vitu kama sukari na akawa anatumia asali mbichi ni vizuri sana pia kupunguza mafuta mengi kwenye chakula na apendelee kutumia mafuta ya mimea kama soya, alizeti n.k, na pia kupendelea kula vyakula halisi (visivyozindikwa)kama matunda fresh, juis fresh, n.k nafikiri ataona mabadiliko mwenyewe.
Asante sana kwa kurudi kutupa 'feedback' ya maendeleo ya nduguyo. Ubarikiwe.