Thanks to technology, kazi ya utongozaji inakuwa rahisi kila siku

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Madomo zege na watu wengine wa kawaida technolojia inazidi kuturahisishia mambo kila kukicha, sio katika maisha ya kawaida ya kila siku hadi kwenye utongozaji.

Nakumbuka zamani ulikuwa unatongoza mtu miezi 6 hadi mwaka bado hujawa nae.Kazi ya kutongoza sio mchezo, kumshawishi mtu mzima na akili zake hadi akukubalie.

Whatsapp, Facebook, Badoo nk zimeahirisha maisha, kazi kubwa ni kupata namba ya mtu tu, ukishaipata kazi imeisha. Hii mitandao imeondoa shida ya kuona aibu, shida ya kuviziana na kufuatana miezi 6.

Kwa tekinolojia ya sasa ukishindwa kupata mwanamke utakua sio udomo zege huo, unahitaji maombi ya kufunga na kulia, tena maombi ya mnyororo.

Ishukuriwe teknolojia.
 
ukipata namba tu tu mchezo umekwisha
 
Tena ukimuendea taratibu yani kama hunashida nae hivi, huna haraka nae, utajipigia mapemaaa
 
sijui sie wagoni maisha yetu yangekuaje bila hii mitandao aiseee
 
Naomba kujua kuhusu hiyo badoo kwa aliyewahi kutumia na kufanikiwa kupata mke. nimejaribu naona kuna kulipia kwa ksh
 
Teknolojia haikuanzishwa mahususi kwa ajili hiyo lakini, sema waTanzania mmezoea kuchakachua kila kitu!
 
Sikuhiz ukimtongoza dem face2face sio heshima. Heshima mtongozee Whatsapp
 
Sikuwa najua Hilo....! Nitafanyia kazi!!!
 
kweli kabisa teknolojia inaendelea kufanya kazi

Umeona eeh, enzi zile mtu alikuwa anajitetea niko mbali na benki, sijabeba ATM nk.

Siku hizi unaweza kutoa hela benk kuja kwenye simu au kutoka kwenye simu kwenda benk.
 
Umeona eeh, enzi zile mtu alikuwa anajitetea niko mbali na benki, sijabeba ATM nk.

Siku hizi unaweza kutoa hela benk kuja kwenye simu au kutoka kwenye simu kwenda benk.
na kutoa kwenye simu kuja kwa miss hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…