Viongozi wao walikuwa ni wezi na wasiofuata haki. Misri bado wanatawaliwa na jeshi, Libya ukanda na ukabila unawamaliza na kuwa na amani 100% itachukua muda sana. Tunisia ni mfano mzuri wa jinsi ya kung'oa udikteta. Algeria wamegawanyika nusu kwa nusu na utawala uliopo bado una support kubwa kulinganisha na wanamageuzi.
Bahrain na Syria ukandamizwaji ni mkubwa na inaonyesha jinsi nchi za magharibi zilivyo wanafiki.Morocco na Yemen wana mifumo tofauti ila changes zitakazofanyika nazo bado zitakuwa nusu nusu kutokana na Cultures zao kuwa superior to the government apparatus (Monarchy and Tribal leaders respectively).
Tanzania ni nchi ya kidemokrasia ghafi, Demokrasia yetu inabidi iimarishwe kwa kubadilisha katiba na mfumo wa uongozi (Power of the executive) na kuboresha mahakama zetu kwa kuzipa uhuru kamili na kuhakikisha mahakama kuu inateuliwa na rais na kupitishwa na bunge (mawazo yangu tu), kuuimarisha muungano kwa kuwa na serikali moja, au kuuengua muungano kabisa kwani hii kitu itakuju kutugharimu sana tukikaa kimya. Tusitegemee jeshi au polisi kuzima ari ya wananchi kutaka kujua hatma ya muungano.
Tunachojifunza watu wengi hasa wa CDM hawatakwambia, viongozi wenye mvuto wa CDM wameonyesha si chini ya mara mbili, kutaka kujaribu mabadiliko ya nguvu. Hawana support ya umma kwa hili, na mawazo yao ya kujitenga (divide and rule) hayana mashiko kwa watanzania wengi. Wasubiri uchaguzi wa 2014? na 2015, ila tuhakikishe tuna katiba iliyokubalika na uchaguzi huru utaosimamiwa na tume huru wakati tuna mahakama zinazoheshimika na kukubaliwa na wananchi.
Militancy wanayojaribu kina Lema, Heche, Nassari, Slaa (na Lissu kidogo ingawa ameacha) hazitaatufikisha popote pale. Nitukane unavyopenda ila usinishikie silaha, kwani hujui what I'm packing. Hata mitaani kuna watu wanaanza kuwa too aggressive wakijua wewe ni CCM, let's just stop this nonsense, it's not gonna work.