kajekudya
JF-Expert Member
- Sep 24, 2015
- 2,466
- 4,916
Katika harakati zake za maisha tangu siku yake ya kwanza, binadamu amepitia mambo mengi ya kijamii na kiuchumi. Moja ya mambo hayo ni Vita, kwa wanahistoria Kuna Vita nyingi maarufu na zisizo maarufu zimewahi kupiganwa kuanzia zile za kibiblia Kama ile ya Daudi dhidi ya Jabali Goliati Hadi zile za huku kwetu Kama a hundred years war Kati ya Wamarekani Kaskazini na Wamarekani kusini au Six days war Kati ya Wazayuni na Waarabu, lakini funga kazi watakwambia ni First and Second Word Wars.
Yote kwa yote Kuna Vita moja huwezi kusikia watu wakiimba Sana, hi ni ile iliyopewa jina maalufu ya "the battles of Solferino", Vita amabayo ilikuja kuleta Mapinduzi makubwa kwa kuweka misingi ya kuregulate baadhi ya mambo katika uwanja wa Vita, Vita yenyewe ilikuwaje Basi!? na ilikuwa Kati ya Nani na Nani!?
Hi ni Vita iliyopiganywa kwa mda wa siku moja Huku ikiacha maelfu ya Askari wakipoteza maisha na maelfu wakiwa majeruhi ilitokea mnamo June 24 Mwaka 1859 ikihusisha Austria iliyokuwa chini ya Emperor Franz Joseph akiwa na miaka 29 tu wakati huo, dhidi ya Ufaransa kwa pamoja na Sardinia(Itally), Ufaransa ikiongozwa na Napollean III huku Sardinia ikiongozwa Emmanuel II na ilihusisha zaidi ya wapiganaji 270000, 130000 kwa upande wa Austria na 14000 kwa upande wa Ufaransa na Sardinia kwa pamoja na Hadi Vita inaisha huku Austria akinyosha mikono alikuwa tayari amepoteza wapiganaji 13000 achilia mbali upande wa pili na majeruhi.
Mda mfupi baada ya Vita hii alipita katika eneo mtu ambaye alikuja kuleta mabadiliko na kuifahamisha dunia juu ya tukio hilo baya, huyu ni Jean Henry Dunant ambaye alikuja kuandika kitabu maarufu Cha "the Memory of Solferino", kutokana na madhira aliyoshuhudia hasa kwa majeruhi wa Vita ndipo alipoanza kampeni kabambe za kuhakikisha kunakuwa na taratibu zinazosimamia wapiganaji katika uwanja wa vita.
Na mafanikio yalianza kuonekana miaka ya 1860 ambapo liliundwa Shirika la Msalaba mwekundu( the International Red Cross) na first Geneva Convention ilisainiwa, zote zikiwa na malengo ya kuweka baadhi ya misingi ya kuzingatia wakati wa Vita mfano kuruhusu majeruhi watibiwe, nk.Baadae harakati za Henry Dunant zilikuja kupata msukumo zaidi baada ya Vita kuu ya pili ambapo zilizainiwa Conventions nyingi Sana lakini zote zikichukua misingi na maudhui Yale Yale kutoka kwa Henry Dunant ambaye naye alishawishika kuanzishwa harakati hizo kutokana na kile alichpkiona kwenye "the battles of Solferino"
Leo ukigoogle utakutana na Geneva Conventions nyingi na protocols zake Kama Vile First Geneva Conventions for the Amelioration of Conditions of the Wounded and Sick Armed Forces on the Field 1949, Third Geneva Convention Relative to the Treatment of the Prisoners of Wars 1949, 4th Geneva Convention Relative to the protection of the Covilian Persons in time of War 1949, bila Shaka hii ya 4 ndo ilikuwa ikimuhenyesha Jean Pieery Bemba pale The Hegue kwa makosa yalifanywa na kundi lake la MLC pale Africa ya Kati alipowapeleka wapiganaji wake kwenda kumsaidia aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo Jean Pattase aliyekuwa akihenyeshwa vibaya na Jean Franco Bozize amabaye alikuja baadae fanikiwa kumpindua, sasa wale wapigaji badala ya kupigana wao wakaenda kuiba Mali za watu na kufanya ubakaji, then Bemba akashitakiwa chini ya principle ya Superior Rensponsibility!
Kwa ufupi hizi vurugu zote za kuanzishwa kwa ICC na hatimaye watu kuburutwa huko zinapata msingi wake katika Vita hii japo yamekuwa yakifanyika mabadiliko kadha wa kadha kupitia Protocols mbalimbali kulingana na jinsi dunia inavuobadilika na medani za Vita zinavyobadilikakupelekwa. Hivyo tunaweza tukasema japo hii vita watu hawaiandika Wala kuisema Seema lakini ni miongoni mwa Vita ambazo zimeleta Mapinduzi makubwa katika viwanja vya mapambano.