The beauty of Democracy in Tanzania

The beauty of Democracy in Tanzania

ProMagufuli

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2021
Posts
253
Reaction score
270
Habari wadau, ni matumaini yangu mko vyema kabisa,

Kwa jina naitwa ProMagufuli.

Napenda kuleta hoja kama kichwa kinavyosema.

Kufuatia uchaguzi wa serikali za mitaa tumeweza kujionea yaliyotokea. Umefanyika uporaji mkubwa wa demokrasia.

Sasa kama wanajamii forum ni nini kifanyike ili kuweza kuzuia hii hali isije ikajirudia kwenye uchaguzi mkuu. Nadhani kama taifa tumejifunza yaliyotokea 2019 na 2020.

Sasa watu binafsi, asasi za kiraia Wana mpango gani ili kunusuru taifa na yalitokea nyuma yasijitokeze tena 2025.

Najaribu kuwaza kwa sauti, hakuna namna inaweza kufanyika ili haya mambo yafikie ukomo. Ni nini kinatukwamisha Kama taifa

Mwisho nipende kutoa rai yangu kwa vyama vya siasa viache ubinafsi waangalie maslahi mapana ya nchi yetu.

Waweze kuwa na msimamo wananchi wa kuwaunga mkono wapo.

Pia wasichoke kuwapigania wajinga. Ili kuweza kumshinda CCM inapaswa tuungane kama taifa. Tukiendelea kuwa kimakundi ni ngumu kutoboa tuache kulalamika.

Kwa sasa Niko Mvumi Dodoma, muwe na jioni njema.
1733011528109.jpg
 
Habari ProMagufuli na wadau wote. Asante kwa kuleta mada hii muhimu.

Umeweka wazi kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa umetuonyesha mapungufu makubwa katika demokrasia yetu. Ni kweli tumeona uporaji mkubwa wa kura na ukiukwaji wa haki za wananchi.

Hebu tuchambue kwa kina zaidi na tutafute suluhu:
1. Ufahamu wa kina wa tatizo:
* Tujifunze kutoka kwa makosa: Tumejifunza mengi kutoka kwa uchaguzi wa 2019 na 2020. Tujaribu kuelewa ni wapi hasa mambo yalikwenda kombo.
* Tufanye utafiti: Tutafute taarifa zaidi kuhusu ukiukwaji uliotokea na sababu zake. Hii itatusaidia kupanga mipango bora ya kuzuia kurudiwa kwa matukio kama haya.

2. Ushirikiano wa wadau wote:
* Wananchi: Tuwe macho na tuhakikishe tunajiandikisha kupiga kura. Tujifunze haki zetu na tuzitetee.
* Asasi za kiraia: Zifanye kazi ya kuhamasisha wananchi, kufuatilia uchaguzi, na kutoa elimu kuhusu demokrasia.
* Vyama vya siasa: Viwe na viongozi imara na mipango kabambe ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uhuru na haki.
* Vyombo vya usalama: Vifanye kazi kwa uadilifu na kuhakikisha usalama wa kila mwananchi wakati wa uchaguzi.

3. Mabadiliko ya kimfumo:
* Sheria: Turekebishe sheria zetu ili ziweze kulinda demokrasia na kuzuia ulaghai katika uchaguzi.
* Tume za uchaguzi: Tuzifanye kuwa huru na zenye uwezo wa kufanya kazi bila kuingiliwa na vyama vya siasa au serikali.
* Vyombo vya habari: Viwe huru na kutoa taarifa sahihi kuhusu uchaguzi.

4. Teknolojia:
* Kutumia teknolojia: Tujaribu kutumia teknolojia ili kuimarisha mfumo wa uchaguzi. Kwa mfano, kutumia biometrics ili kuzuia kura za kipande.

Kwa ufupi, ili kuzuia marudio ya matukio haya, tunahitaji:
* Uelewa wa pamoja: Kila mmoja wetu aelewe umuhimu wa demokrasia na athari za ukiukwaji wake.
* Ushirikiano: Tushirikiane wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa.
* Mabadiliko ya kimfumo: Turekebishe mifumo yetu ili iweze kutuhudumia vyema.
Ushauri kwa vyama vya siasa:
Ushauri wako kwa vyama vya siasa ni mzuri sana. Ni kweli, vyama vinapaswa kuacha ubinafsi na kuzingatia maslahi ya taifa. Wanapaswa pia kuimarisha uhusiano wao na wananchi.

Wito kwa wote:
Tusikate tamaa. Tuzidi kupigania demokrasia yetu. Tukishirikiana na kuwa na subira, tutaweza kufikia lengo letu la kuwa na nchi yenye demokrasia imara.

Maswali ya kufikiria:
* Ni mikakati gani mingine tunaweza kuitekeleza ili kuzuia ulaghai katika uchaguzi?
* Je, tunaweza kuanzisha kampeni ya uhamasishaji wa wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi?
* Jinsi gani tunaweza kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinatoa taarifa sahihi na za kuaminika kuhusu uchaguzi?

Nimefurahi sana kuona kuwa unavutiwa na masuala haya muhimu. Tunaweza kuendelea kujadili na kupata suluhu za pamoja.

Kumbuka: Umoja ndio nguvu. Tukishirikiana, tutaweza kujenga Tanzania bora zaidi.
Asante.​
 
Tuachane na siasa, tujadili mpira tu
 
Habari ProMagufuli na wadau wote. Asante kwa kuleta mada hii muhimu.

Umeweka wazi kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa umetuonyesha mapungufu makubwa katika demokrasia yetu. Ni kweli tumeona uporaji mkubwa wa kura na ukiukwaji wa haki za wananchi.

Hebu tuchambue kwa kina zaidi na tutafute suluhu:
1. Ufahamu wa kina wa tatizo:
* Tujifunze kutoka kwa makosa: Tumejifunza mengi kutoka kwa uchaguzi wa 2019 na 2020. Tujaribu kuelewa ni wapi hasa mambo yalikwenda kombo.
* Tufanye utafiti: Tutafute taarifa zaidi kuhusu ukiukwaji uliotokea na sababu zake. Hii itatusaidia kupanga mipango bora ya kuzuia kurudiwa kwa matukio kama haya.

2. Ushirikiano wa wadau wote:
* Wananchi: Tuwe macho na tuhakikishe tunajiandikisha kupiga kura. Tujifunze haki zetu na tuzitetee.
* Asasi za kiraia: Zifanye kazi ya kuhamasisha wananchi, kufuatilia uchaguzi, na kutoa elimu kuhusu demokrasia.
* Vyama vya siasa: Viwe na viongozi imara na mipango kabambe ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uhuru na haki.
* Vyombo vya usalama: Vifanye kazi kwa uadilifu na kuhakikisha usalama wa kila mwananchi wakati wa uchaguzi.

3. Mabadiliko ya kimfumo:
* Sheria: Turekebishe sheria zetu ili ziweze kulinda demokrasia na kuzuia ulaghai katika uchaguzi.
* Tume za uchaguzi: Tuzifanye kuwa huru na zenye uwezo wa kufanya kazi bila kuingiliwa na vyama vya siasa au serikali.
* Vyombo vya habari: Viwe huru na kutoa taarifa sahihi kuhusu uchaguzi.

4. Teknolojia:
* Kutumia teknolojia: Tujaribu kutumia teknolojia ili kuimarisha mfumo wa uchaguzi. Kwa mfano, kutumia biometrics ili kuzuia kura za kipande.

Kwa ufupi, ili kuzuia marudio ya matukio haya, tunahitaji:
  • Uelewa wa pamoja: Kila mmoja wetu aelewe umuhimu wa demokrasia na athari za ukiukwaji wake.
  • Ushirikiano: Tushirikiane wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa.
  • Mabadiliko ya kimfumo: Turekebishe mifumo yetu ili iweze kutuhudumia vyema.
Ushauri kwa vyama vya siasa:
Ushauri wako kwa vyama vya siasa ni mzuri sana. Ni kweli, vyama vinapaswa kuacha ubinafsi na kuzingatia maslahi ya taifa. Wanapaswa pia kuimarisha uhusiano wao na wananchi.

Wito kwa wote:
Tusikate tamaa. Tuzidi kupigania demokrasia yetu. Tukishirikiana na kuwa na subira, tutaweza kufikia lengo letu la kuwa na nchi yenye demokrasia imara.

Maswali ya kufikiria:
  • Ni mikakati gani mingine tunaweza kuitekeleza ili kuzuia ulaghai katika uchaguzi?
  • Je, tunaweza kuanzisha kampeni ya uhamasishaji wa wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi?
  • Jinsi gani tunaweza kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinatoa taarifa sahihi na za kuaminika kuhusu uchaguzi?

Nimefurahi sana kuona kuwa unavutiwa na masuala haya muhimu. Tunaweza kuendelea kujadili na kupata suluhu za pamoja.

Kumbuka: Umoja ndio nguvu. Tukishirikiana, tutaweza kujenga Tanzania bora zaidi.
Asante.​
Tatizo liko kwenye jamii yetu ni jamii ya kanyaga twende jamii ambayo haiwezi kuchakata fikra chanya na hasi
 
Habari wadau, ni matumaini yangu mko vyema kabisa,

Kwa jina naitwa ProMagufuli.

Napenda kuleta hoja kama kichwa kinavyosema.

Kufuatia uchaguzi wa serikali za mitaa tumeweza kujionea yaliyotokea. Umefanyika uporaji mkubwa wa demokrasia.

Sasa kama wanajamii forum ni nini kifanyike ili kuweza kuzuia hii hali isije ikajirudia kwenye uchaguzi mkuu. Nadhani kama taifa tumejifunza yaliyotokea 2019 na 2020.

Sasa watu binafsi, asasi za kiraia Wana mpango gani ili kunusuru taifa na yalitokea nyuma yasijitokeze tena 2025.

Najaribu kuwaza kwa sauti, hakuna namna inaweza kufanyika ili haya mambo yafikie ukomo. Ni nini kinatukwamisha Kama taifa

Mwisho nipende kutoa rai yangu kwa vyama vya siasa viache ubinafsi waangalie maslahi mapana ya nchi yetu.

Waweze kuwa na msimamo wananchi wa kuwaunga mkono wapo.

Pia wasichoke kuwapigania wajinga. Ili kuweza kumshinda CCM inapaswa tuungane kama taifa. Tukiendelea kuwa kimakundi ni ngumu kutoboa tuache kulalamika.

Kwa sasa Niko Mvumi Dodoma, muwe na jioni njema.View attachment 3166689
Kwa vyama vya siasa kuungana hapo sioni kama itasaidia. Kumbuka kwamba kuna vile vyama 14, ambavyo vinajiita ni vya upinzani, lakini behaviour yake ni kama vyama saidizi vya CCM au vinavyounga mkono CCM. Kuungana na vyama hivyo (na vikisikia kuna mpango kama huo vitajisogeza karibu) ni kupalaganyika. Hili ndilo tatizo ninaloliona. Kwa upande wangu, chama cha upinzani ni kile kinachotoa 'challenge' kwa serikali ili iweze kuwajibika zaidi kwa wananchi, siyo ambacho mara nyingi kinaunga mkono mambo ambayo yanakandamiza upinzani nchini.
 
Nini kifanyike, ili kuondoa hio shida?
Elimu elimu anza wewe kwenye família yako, waelekeze kwamba tunao wapa dhamana huahirisha kufikiri kwa nafsi a.k.a kujizima data tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo

Washika tonge hukengeuka, hutumia unyumbu wa kisiasa

Unyumbu wa kisiasa ni tabia ya wanaopewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga kwa viongozi wao bila utii, (unafiki)

Someni pia kuhusu "ostracism" mtanishukuru sana
 
Kwa vyama vya siasa kuungana hapo sioni kama itasaidia. Kumbuka kwamba kuna vile vyama 14, ambavyo vinajiita ni vya upinzani, lakini behaviour yake ni kama vyama saidizi vya CCM au vinavyounga mkono CCM. Kuungana na vyama hivyo (na vikisikia kuna mpango kama huo vitajisogeza karibu) ni kupalaganyika. Hili ndilo tatizo ninaloliona. Kwa upande wangu, chama cha upinzani ni kile kinachotoa 'challenge' kwa serikali ili iweze kuwajibika zaidi kwa wananchi, siyo ambacho mara nyingi kinaunga mkono mambo ambayo yanakandamiza upinzani nchini.
Au tususie uchaguzi mpaka pale misingi Bora ya demokrasia ikiwekwa.
Tume huru na usimamizi huru wa uchaguzi. Maana kuendelea kushiriki ni kama kuzidi kuwabariki CCM na madudu yao.

Ila wajaribu kuungana, na vyama ambavyo vinaonekana ni saidizi kwa CCM visiruhusiwe kuungana. Au la kuwe na msemaji mmoja hata baada ya uchaguzi, hata ikitokea vikajiengua msimamo wao null
 
Maswali ya kufikiria:
  • Ni mikakati gani mingine tunaweza kuitekeleza ili kuzuia ulaghai katika uchaguzi?
  • Je, tunaweza kuanzisha kampeni ya uhamasishaji wa wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi?
  • Jinsi gani tunaweza kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinatoa taarifa sahihi na za kuaminika kuhusu uchaguzi?
Taratibu ndugu, wale watu watakunyorosha!
 
Au tususie uchaguzi mpaka pale misingi Bora ya demokrasia ikiwekwa.
Tume huru na usimamizi huru wa uchaguzi. Maana kuendelea kushiriki ni kama kuzidi kuwabariki CCM na madudu yao.

Ila wajaribu kuungana, na vyama ambavyo vinaonekana ni saidizi kwa CCM visiruhusiwe kuungana. Au la kuwe na msemaji mmoja hata baada ya uchaguzi, hata ikitokea vikajiengua msimamo wao null
Mambo yote haya kufanyika yanategemea msukumo wa wananchi, maana wao ndio wanaoweza kuamua wafanye hiki au kile, wanapenda hiki kwanza, na kile baadaye. Mfano, kama maandamano yaliyoitishwa na Chadema yangekuwa yanatokana na msukumo wa wananchi yangefanikiwa kwa maana kwamba watu wengi wangeshiriki. Lakini badala yake wananchi walibaki kama 'onlookers' kama unavyoweza kuangalia mchezo wa kuigiza au mpira kwenye TV ukiwa nyumbani, maana mchezo wa kuigiza au mpira haukuhusu, unaangalia tu kuburudisha akili.
 
Jambo lingine ni kwamba mambo yote hayawezi kukamilika kwanza, ndipo tufanye uchaguzi. Kwa vile 'power corrupts' tukifanya hivyo, Yesu atarudi kwa mara ya pili na kukuta tukisubiri uchaguzi huru na wa haki utakaofanyika chini ya tume huru ya uchaguzi. Kinachotakiwa ni utashi wa kisiasa, maana hata tukiwa na Katiba mpya au tume huru ya uchaguzi, lakini hakuna utashi wa kisiasa, hakuna atakayejali kuna Katiba mpya au tume huru. Hivyo, utaona kwamba mambo yote haya yanategemeana: utashi wa kisiasa, kuwa na tume huru ya uchaguzi (isiyolalamikiwa) na katiba mpya (ambayo haijachakachuliwa?).
 
Lakini mimi nadhani kwenye suala la maandamano, Walioitisha walipaswa kuitisha ya non stop, wangeendelea tu hata kama ni wachache baadae wananchi wangewaunga mono, tatizo na wao hawama uvumilivu.

But sijajua ugumu unakuwa wapi exactly na kwanini hawawezi kuendeleza maandamano
 
Bora tusubiri yakamilike ndio tufanye uchaguzi. Maana kwa SASA hata tukifanya ni upotezaji wa rasilimali na muda maana outcome yake inajulikana.

Bora kusubiri mpaka Yesu arudi kuliko kushiriki uchaguzi ambao mnajua hamuwezi kushinda.
 
Lakini consequences za kuendelea na utaratibu wa sasa hazitakuwa rafiki pia.
 
Lakini mimi nadhani kwenye suala la maandamano, Walioitisha walipaswa kuitisha ya non stop, wangeendelea tu hata kama ni wachache baadae wananchi wangewaunga mono, tatizo na wao hawama uvumilivu.

But sijajua ugumu unakuwa wapi exactly na kwanini hawawezi kuendeleza maandamano
Wao kama wao peke yao watadhibitiwa tu. Maandamano ambayo si rahisi kuyadhibiti ni yale ya wananchi wenyewe, na haya kwa sasa hayawezekani kwa sababu wananchi wanaonekana wasioguswa (indifferent) na malalamiko yanayotolewa na Chadema au vyama vya upinzani kwa jumla.
 
Pia wasichoke kuwapigania wajinga. Ili kuweza kumshinda CCM inapaswa tuungane kama taifa. Tukiendelea kuwa kimakundi ni ngumu kutoboa tuache kulalamika.
Siku hizi ujinga mtaani umepungua umehamia kwenye tume na polisi ambao wamekubali kugeuzwa kuwa punda wa kubebeshwa kura fake na kujaza kwenye masanduku ya kura.
 
Wao kama wao peke yao watadhibitiwa tu. Maandamano ambayo si rahisi kuyadhibiti ni yale ya wananchi wenyewe, na haya kwa sasa hayawezekani kwa sababu wananchi wanaonekana wasioguswa (indifferent) na malalamiko yanayotolewa na Chadema au vyama vya upinzani kwa jumla.
Basi tungojee Neema ya Mungu
 
Back
Top Bottom