Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Leo kwa heshima kubwa naomba nikupe simulizi ya ndugu watatu kutoka Uingereza ambao walitupatia vionjo matata sana katika nyimbo zao, ni kaka watatu ambao ukiwatazama utaona ni kama hawafahamu chochote katika muziki ila wakianza kurekebisha sauti na kutoa mashairi yao kwa hakika utabakia mdomo wazi, kaka watatu ambao walikuwa na uwezo wa ajabu wa kuzibadilisha sauti zao kuendana na ala husika ya muziki, kuanzia mwishoni mwa mwaka 1960 mpaka mwishoni wa miaka ya 1970 walipata umaarufu mkubwa sana. Karibu sana leo nikupe simulizi pana ya bendi kutoka Uingereza ambao ilijipatia jina la The Bee Gees, wengine wamewapatia jina la The Disco Kings, Mashabiki wao waliopo Ulaya waliwabatiza jina la Britain's First Family of Harmony, na dunia inawatambua kama ndo The Kings of Dance Music.
Chorlton, Manchester, Uingereza ndo mahali ambao kaka hawa watatu kutoka familia ya Gibb, sehemu ambayo waliishi mpaka mwishoni mwa 1950, na kabla ya kanzishwa kwa bendi ya The Bee Gees, kaka hawa walianzisha bendi yao ya mwanzo kabsa ambayo iliitwa Rattlesnakes, wakiwa na bendi ya Rattlesnakes walikutana na changamoto ya kukosa eneo la kufanyia maonyesho yao kitaalamu ukumbi kutokana na gharama kubwa ya kukodisha sehemu. Barry, Robin, Maurice, wakiwa na marafiki zao Paul Frost pamoja Kenny Horrocks yaani jeshi la watu watano waliwatia wazimu watu kwa uwezo wao wa kuimba.
Mara kadhaa walifanya kuimba wakiwa nje huku watu wakionesha kuwapenda sana, wakati mmoja recorder yao ya shellac 78-RPM kikipata hitilafu hivyo ikawabidi kuanza kuimba mubashara pasipo kutumia recorder, na hii ikawafanya wawe wazuri zaidi kwani sauti zao ndo ziliwavutia zaidi hadhira. Lakini Mei 1958, Frost pamoja na Horrocks waliondoka kwenye bendi ya Rattlesnakes ili wakatafute changamoto sehemu zingine, na hapa ndipo walipobakia ndugu watatu, ambao walibadilisha jina bendi yao na kuipa jina la Wee Johnny Hayes and the Blue Cats huku Kaka yao Barry akiwa anatambulika kwa AKA ya Johnny Hayes.
Agosti 1958 familia ya Gibb ilihama na kwenda Australia na kuweka makazi huko Redcliffe, Queensland Kaskazini mashariki mwa Brisbane, Barry na wenzake wakiwa ni mabarobaro walianza kuimba mtaani ili kuchangisha fedha za kuwaendeleza zaidi kimuziki. Basi siku moja wakiwa wanaimba zao na watu wanawatunza, Bwana mmoja aliyekuwa anaitwa Bill Goode aliwasikia na kuwapa kibarua ndugu hawa watatu ya kuwaburudisha watu wa Redcliffe Speedway, kisha baadaye aliona vijana wana moyo na talanta za kuimba hivyo akawapatia connection na kuwaunganisha kwa Bill Gates, kwa hakika walivuna pesa nyingi wakiwa wanatumbuiza nyimbo zao pale Redcliffe Speedway. Gates alibadilisha bendi hii na kuipa jina la BGs na baadaye kuitwa rasmi jina la Bee Gees ikiwa ni baada ya kuchukua herufi za mwanzo za majina ya Goode na Barry. Jina la Bee Gees halikuwa na uhusiano wowote wa ndugu wote watatu bali ni Barry pekee.
Miaka kadhaa baadaye, walipata nafasi ya kwenda kuimba kwenye kumbi za wageni katika fukwe za Queensland ambapo pia walipata umaarufu mkubwa na pesa. Barry aliona nafasi na kumfuata nyota wa Australia Col Joye ambaye aliwasaidia kupata mchongo wa kurekodi mwaka 1963 kwenye record label ya Leedon Records ambayo ilikuwa chini ya Festival Records na hapo wakaanza kutumia rasmi jina la Bee Gees, watatu hao walitoa nyimbo tatu mwaka 1963 huku Barry akitoa msaada wa uandishi wa nyimbo kwa wasanii wengine wa Australia. Mwaka 1962 kundi hili lilipata nafasi ya kuwa sehemu ya tamasha la Chubby Checker lililofanyika kwenye uwanja wa Sydney; hii ilizidi kuwapatia ujasiri wa kutoboa zaidi.
Kuanzia mwaka 1963 mpaka 1966 familia ya Gibb ikapata kuishi huko Sydney, na kabla ya kifo chake, Robin Gibb aliandika na kurekodi wimbo wa Sydney ambao unaelezea historia na Maisha yao yalivyokuwa pale Sydney, shida na raha hususani upande wao wa mafanikio waliyoyapata ndani ya Australia, nyimbo hii iliachiwa rasmi ikiwa ni moja ya nyimbo za Robin katika albamu yake ya 50 St. Catherine's Drive, makazi hayo ambayo walipata kukaa yalibomolewa mwaka 2016.
Wimbo wa Wine and Women ambao ulitoka 1965 ulikuwa wimbo wa kwanza kwa kundi kuuimba mubashara jukwaani, kufikia 1996 walianza kushuka kimauzo na record label mama yao ya Festival Records ilikuwa mbioni kuvunja mkataba na The Bee Gees, siku moja wakiwa wanapiga misele ya wakakutana na Nat Kipner ambaye wakati huo alikuwa ni mwandishi na mtunzi mzuri sana wa muziki, lakini pia Kipner alikuwa ni mzalishaji wa muziki pamoja na mjasiriamali, na kwa bahati nzuri wakati The Bee Gees wanakutana na Kipner, ndo ulikuwa wakati ambao Kipner amekula shavu la kuwa A&R manager wa record label ya Spin records, basi baada ya kuona kuwa kundi la The Bee Gees bado lina madini mengi sana, Kipner alikubali kuwa manager wao na kuwachukua kutoka Festival Records na kuwapeleka Spin Records kwa kigezo cha Festival Records kubaki na hakimiliki ya nyimbo ambazo The Bees Gees walizitoa wakiwa Australia.
Kipner akamtafuta guru mmoja fundi kwenye kutengeneza ala na uandaaji wa midundo pamoja na sauti za vyombo kadhaa, huyu ni Ossie Byrne ambaye alifanya kazi bega kwa bega akiwa na Kipner. Na kwa upekee wa ajabu The Bees Gees walipatiwa nafasi muda wowote ya kurekodi na kuandika pamoja na kuandaa mashairi wakiwa pale St Clair Studio ambayo ilikuwa ni ofisi ya Bwana Mkubwa Byrne, The Bees Gees walitumia baraka hii kwa muda wa zaidi ya miezi saba.
Kwa mujibu wa The Bees Gees kwao kukutana na watu wawili hawa (Kipner pamoja na Byrne) ilikuwa ni kama kuokota embe kwenye mfenesi, na iliwajenga sana katika sanaa yao na walijifua zaidi kwani Byrne aliwapatia mpaka funguo kuwa wao wakitaka kuwasha moto basi wako huru muda wowote siku yoyote. Ni katika kipindi hiki ndipo The Bees Gees waliandika nyimbo kali zaidi katika Maisha yao ya muziki, mfano, wimbo wa "Spicks and Specks" ambapo kuna mashairi ya Where is the light................... That would play.................. In my streets............. And where are the friends......... I could meet, safi sana! Siku ambayo wanaweka sauti kwenye ala ya muziki, Byrne alisisimka sana kiasi kwamba aliwaomba aweke kionjo cha tarumbeta kidogo. Kitu kikubwa ambacho Byrne aliwafundisha ndugu hawa watatu ni kuhusu ushirikiano kati yao na wasanii wengine, The Bees Gees walifanya kazi pamoja na bendi ya Steve & The Board katika kazi zao nyingi.
Katika shamba lolote lenye kumea vizuri lazma magugu yatokeze, ndivyo ambavyo bendi hii ya The Bees Gees ambao waliona mafanikio yanachelewa kwani walitumia nguvu na maarifa mengi katika kutoa kazi zao za Sanaa, hivyo Januari 4 1967 asubuhi walianza safari yao ya kurudi Uingereza wakiwa wanyonge kweli, lakini Ossie Byrne hakuwaacha na aliamua kuungana nao, safari ikaanza huku macho yao yakilengalenga machozi na huzuni, ghafla kidogo alipita dogo mmoja aliyekuwa akiuza magazeti basi Barry akanunua gazeti moja la Go-Set ili apate kufahamu kinachoendelea.
Go-Set lilikuwa ni gazeti maarufu sana ndani ya Australia ambalo lilikuwa likiangazia masuala ya musiki, basi akasoma kurasa za mwanzo ila alipofika kati kati alishangaa kuona sehemu imeandikwa "Spicks and Specks" the "Best Single of the Year", mboni zake za macho zikawa kubwa kama vile mjusi amebanwa na mlango, akaona labda uchovu wa safari na kuwaonesha ndugu zake, na wao wakashangaa kuona kuwa wimbo wao wa "Spicks and Specks" ndo umekuwa wimbo bora wa mwaka (Kumbuka kipindi hicho hakuna Twitter wala Facebook, au Reels za Instagram, kifupi taarifa zilikuwa hazisambai kwa wepesi kama ilivyo sasa). Basi mioyo yao ikajawa na furaha sana kuona kuwa kila wanachokifanya kinaonekana kwa hadhira, kwa mujibu wa Barry, aliona Kaka zake wakitoa machozi ya furaha kwa kuona taarifa ile.
Kabla hawajaanza safari yao ya kurejea Uingereza, Hugh Gibb aliwahi kutuma demo kwa Brian Epstein ambaye alikuwa ni manager wa bendi ya Beatles na Mkurugenzi wa NEMS ambayo ilikuwa ni Duka la Muziki ndani ya Uingereza, Epstein aliposikiliza aliona kuwa hawa mabwana wadogo ni mafundi haswa hivyo akazituma kwenda kwa Robert Stigwood ambaye ndo alikuwa ametoka kujiunga na NEMS. Naye aliposikiliza akazipenda sana talanta hizi kwa hakika.
Februari 1967 Stigwood akaandaa nafasi ya The Bees Gees kufanya yao mbele yake, The Bees Gees waliimba sauti zao pasipo kutumia msaada wa chombo chochote mpaka Stigwood alidhani hawatoi sauti, kuna wakati aliuza kama kuna mtu amewasha redio au ni sauti zao (Ni ajabu sana!) Kiukweli lingekuwa kosa kubwa kuziba riziki kwa vijana hawa, hivyo Stigwood aliwasaidia The Bees Gees kuingia makubaliano ya miaka mitano na Polydor Records kwa kazi zao ndani ya Uingereza, huku Atco records wao wakisimamia kazi za The Bees Gees ndani ya Marekani. Punde si punde kazi kubwa ikaanza kwa kuandaa albamu yao ya kwanza ya kimataifa, mzee wa kazi Stigwood akaandaa kampeni kubwa ya kuitangaza albamu hiyo kimataifa.
Ukimuuliza Stigwood kuhusu bendi hii ya the Bee Gees atakujibu kuwa “the Bee Gees were the most significant new musical talent of 1967” na ilifika kipindi watu walianza kuwashindanisha the Bee Gees na bendi ya the Beatles,`ukamini katika unadishi wa mashairi yao pamoja na upekee sa sauti na ala ya muziki ilitosha kabsa kusema kwamba The Bee Gees walikuwa kwenye mtanange mkubwa na The Beatles, kwa sasa tungesema ulikuwa ni mtanange baina ya Muajentina Lionel Messi dhidi ya Mreno Cristiano Ronaldo, ukisikiliza nyimbo hizi mbili za "I've Got a Feeling" pamoja na How Deep Is Your Love ukapewa nafasi ya kusema ipi ni bora lazma kichwa kiumie kwa dakika zisizopungua kumi ingawa wimbo wa "I've Got a Feeling" kutoka The Beatles ndo unaonekana ni bora kuliko wimbo wa How Deep Is Your Love.
Kabla ya kurekodi albamu yao ya kwanza, kundi hili la The Bee Gees liliongeza vyuma vingine viwili vikali zaidi, hawa walikuwa ni Colin Petersen pamoja na Bwana Mkubwa Vince Melouney. Kiukweli the Bee Gees walikuwa na nafasi yao ya kipekee sana kwani hata Madj walitokea kuvutiwa sana na muziki wao kiasi kwamba kumbi nyingi zikawa zinapiga muziki wa the Bee Gees, hii ilikuwa ni kama bahati mbaya na bahati nzuri kwa wakati mmoja. Ilikuwa hivi, the Bee Gees walirekodi na kutengeneza wimbo wao wa pili kwa jina la New York Mining Disaster 1941. Tatizo wakati vituo vya redio vinapokea kazi hii ili wapate kuicheza hakukuwa na jina la wasanii kwa maana ya cover ya wimbo ilikuwa na jina la la wimbo pekee.
Ajabu zaidi ni kwamba walipocheza wimbo huu walijua moja kwa moja kuwa watunzi na waimbaji ni the Beatles, na kwa kuwa wakati huo the Beatles walikuwa ni maarufu na vipenzi ndani na nje ya Uingereza, vituo vingi vilicheza wimbo huu kiasi kwamba ulipanda chart na kushika nafasi za juu ndani ya Uingereza na Marekani.
The Bee Gees wakaingia tena studio na kupika mzigo mwingine mzito zaidi wa "To Love Somebody", wimbo ambao ulipata mafanikio makubwa kutokana na kiki ya wimbo ule wa New York Mining Disaster 1941, wao The Bee Gees walitumia nguvu kiasi tu kwenye kutangaza wimbo wa "To Love Somebody". Baadaye walitoa wimbo wa "Holiday" wimbo ambao pia ulitembelea nyota ya mafanikio ya New York Mining Disaster 1941, wimbo huu uliachiwa ndani huko Marekani na ulikwea mithili ya nyani mpaka kufika namba 16 kwenye chart.
Albamu yao ya Bee Gees 1st ilifika nafasi ya 7 Marekani huku ikikwea na kufika nafasi ya 8 Uingereza, baada ya kurekodi na kutoa albamu yao hiyo, The Bee Gees walikuwa tayari kwenda kwenye Ukumbi wa Playhouse Theatre, pale makutano ya Northumberland, London kurekodi session yao ya kwanza ya BBC wakiwa na gwiji Bill Bebb, ambapo kwa upekee walifanya onyesho kwa nyimbo tatu.
Mwishoni mwa 1967 walirudi na kwa ajili ya kurekodi albamu yao ya pili, siku nne kabla ya kusherekea kumbukizi ya uzazi wa Kristo, 21 Disemba 1967 katika matangazo mubashara kutoka Kanisa la Liverpool Anglican Cathedral, The Bee Gees walipata nafasi kwenye kipindi maalumu kutoka kwa Mchungaji Edward H. Patey, mwaliko kwa ajili ya maandalizi ya Noel AKA Krismasi, kipindi mubashara cha How On Earth?, pia katika kipindi hicho waliungana pamoja na bendi ya the Settlers pamoja na Kenny Everett ambapo kwa heshima kubwa The Bee Gees waliimba wimbo na utunzi maalumu wa "Thank You For Christmas" sauti zao zilitosha kuteremsha malaika kuja kupata burudani ya kipekee, kisha waliimba nyimbo maarufu za Krismas za "Silent Night", "The First Noel" and "Mary's Boy Child" na kuwashangaza sana watu kwa uwezo wa kutumia sauti zao.
The Bee Gees walianza Januari kwa baraka hakika kwani walipata ziara ya muziki Marekani, ajabu ni kwamba Idara ya polisi ya Los Angeles iliingia kazini kwani ilikuwa ni kama vile The Beatles ndo wamefika Marekani, hivyo ulinzi uliimarishwa zaidi huku umakini mkubwa ukiwekwa katika mapokezi ya The Bee Gees. Februari 1968 waliachia albamu yao ya Horizontal ambao ilipata mafanikio makubwa kama ile albamu ya kwanza, ndani ya albamu hiyo kuna chuma kizito sana cha Massachusetts ambayo ilishika namba moja kwenye chart za Uingereza huku kwa upande wa Marekani ikishika namba 11, kwa mara ya kwanza albamu ya Horizontal ikawa na ala za miondoko ya rock zaidi kuliko albamu za mwanzo, albamu hii ilishika namba 12 kwa Marekani na namba 16 Uingereza, mafanikio ya kipekee sana.
Mafaniko ya albamu ya Horizontal yakafungua njia yao ya kupata mafanikio kwenye nchi za Scandinavia kwa kupata ziara za kimuziki ndani ya Jiji la Copenhagen, pesa zikawa zinamiminika tu kwa mafundi wa muziki kiasi kwamba waligomea ofa ya kuandika muziki kwenye filamu ya Wonderwall.
27 Februari The Bee Gees wakapata shavu jingine la ziara huko Ujerumani ndani ya Kumbi mbili pale Hamburg Musikhalle, na waliunganisha nguvu na maguro 17 wa Massachusetts String Orchestra katika ziara hiyo. Machi mwaka huo huo The Bee Gees wakaungana na Procol Harum ambaye alikuwa na chuma chake kizito sana cha "A Whiter Shade of Pale"katika ziara ya muziki ndani ya Ujerumani, walizuru kwenye kumbi zaidi ya 11 ambapo walifanya maonyesho zaidi ya 18 na kumaliza ziara yao pale Stadthalle, Braunschweig.
Baada ya hapo bendi ikafunga safari na kwenda Uswisi, kwa upendo mkubwa sana walipokelewa na Watoto zaidi ya elfu 5 kwenye uwanja wa ndege pale Zurich, na barabara Watoto walijaa kuwalaki The Bee Gees huku wengine wakiimba kwa furaha kwa kuwaona mubashara The Bee Gees, Polisi walikuwepo ila hawakuwazuia Watoto kwa sababu Watoto waliwapenda sana The Bee Gees.
Machi 17 The Bee Gees walifanya onyesho la "Words" kwenye kipindi cha The Ed Sullivan Show wakiwa na wasanii wengine, Lucille Ball, George Hamilton and Fran Jeffries, hawa sio watu wepesi kabsa kukaa nao karibu enzi hizo kwani kila mtu alikuwa ni fundi kwenye kile ambacho anakifanya. Siku kumi baadaye The Bee Gees walifanya onyesho kwenye ukumbi wa Royal Albert Hall uliopo pale London Uingereza.
Baada ya kufanya ziara na vipindi vya luninga mbalimbali ili kutangaza albamu zao, Vince Melouney aliondoka katika bendi hiyo huku akidai kuwa alitamani zaidi kuimba nyimbo za miondoko ya Blues na sio hiki ambacho kinaendelea, huku wimbo wa "Such a Shame" ukiwa ndo wimbo pendwa kwa Melouney kwani hakuandikwa na mwanafamilia wa Gibb. The Bee Gees walitakiwa kuanza ziara ya wiki saba ya kimuziki ndani ya Marekani kuanzia Agosti 2 1968 ila Julai ya tarehe 27 Robin alipoteza fahamu na kuzimia, alilazwa na hivyo ziara hiyo ilihairishwa. Baada ya Robin kulazwa, bendi ilirudi kazini na kuanza kurekodi na Robin hakuhusika katika kurekodi albamu hiyo ambayo ilirekodika katika studio za Atlantic Studios za pale New York.
Katika familia lazma kuna mmoja ataona wivu ka namna moja au nyingine, hivyo mwaka 1969 Robin aliona kama Stigwood amekuwa akimpa muda mwingi sana na nafasi ya kuwa kiongozi kaka yake Barry, hapa mambo yakaanza kuharibika mdogo mdogo, chuki na wivu wa kijingajinga tu, yaani mtu ni mgonjwa ila badala ya kupigania afya yako bado unafikiria kuwa Kaka yako anapewa kipaumbele (Binadamu bhana).
Mwanzoni mwa 1960 The Bee Gees walifanya maonyesho yao kwenye vipindi vya Top of the Pops pamoja na The Tom Jones Show ambapo waliimba nyimbo za "I Started a Joke" na "First of May" na hii ilikuwa ndo onyesho la mwisho kabla ya Robin kuzira na kuondoka kwenye bendi ya The Bee Gees, wivu wa kijinga sana aisee. Robin aliona ni vyema akapambane kivyake ila sio kuona kaka yake akiwa kiongozi.
Albam iliyofuata ilikuwa ni Masterpeace ambayo baadaye iligawanywa na kuwa na albamu nyingi kwa jina la Odessa, mashabiki wengi wanaitaja albamu hii kuwa ndo albamu bora kutoka kwa The Bee Gees ikiwa na nyimbo kama "Marley Purt Drive" pamoja na"Give Your Best", pia vibao vikali kama"Melody Fair" bila kusahau "First of May".
Kwa mara ya kwanza The Bee Gees Barry, Maurice and Petersen bila Robin walirekodi albamu ya Cucumber Castle huku pia wakifanya onyesho lao la kwanza la Talk of the Town bila Robin, mara kadhaa walimchukua dada yao, Lesley kuchukua nafasi ya Robin. Lakini kuondokwa kwa Robin kuliwavuruga kabsa wengine kwani walianza kupoteza ladha kabsa, kwani Petersen ambaye alikuwa mpiga ngoma mzuri sana naye pia alifukuzwa huku sababu zikiwa ni zile zile, huku Terry Cox akipewa nafasi ya kupiga ngoma.
Baada ya albamu hiyo kutoka mwanzoni mwa 1970 ilionekana wazi kuwa bendi ya the Bee Gees ilikuwa imemaliza mwendo wake, wimbo wa "Don't Forget to Remember" ulikuwa ni chuma kizito sana ndani ya Uingereza ambapo ilishika nafasi ya 2 huku kwa upande wa Marekani ikiweza kufika nafasi ya 73. Kwa bahati mbaya, Disemba mosi 1969, Barry na Maurice wakatengana rasmi ili kila mtu afanya shughuli zake za kimuziki.
Maurice hakulaza damu kwani alianza kurekodi albamu yake binafsi, The Loner albamu ambayo haikutoka ingawa aliachia wimbo wa "Railroad" ambao ulikuwa ni chuma kizito sana. Februari 1970 Barry alijibu mapigo kwa kuingia studio kurekodi albamu yake ambayo pia haikutoka huku kukiwa na wimbo wa "I'll Kiss Your Memory" pamoja na "This Time" ambazo zilipata mafanikio kiasi tu kwa uchache. Robin yeye alikuwa anakwea tu kwenye chart za Ulaya pamoja na Australia akiwa na ngoma yake ya "Saved by the Bell" kutoka kwenye albamu yake ya Robin's Reign. Mpaka hapa ikaonekana kuwa Robin ndo ameweza kusimama akiwa peke yake kuliko kaka zake wawili, Maurice pamoja na Barry.
Ni majira ya asubuhi Robin aliamua kuokoa jahazi za kaka zake hivyo akampigia simu Barry na kumuomba warudi wawe pamoja kama The Bee Gees, na kumuomba kaka yake Maurice kuwa warudishe ladha ya muziki wakiwa kama bendi. Agosti 21 1970 mara baada ya kurudi pamoja Barry aliongea kwa uchungu sana kuwa "are there and they will never, ever part again" huku Maurice akidai "We just discussed it and re-formed. We want to apologise publicly to Robin for the things that have been said.", dogo aliona kuwa wamezingua pakubwa sana hivyo wanapaswa kuomba radhi kwa kaka yao. Na ili kuonesha kuwa moyo wao ni mweupe na hawana kinyongo na Kaka yake Robin, walirekodi nyimbo kadhaa kabla ya Barry hajaungana nao. Wakati huo Barry na Robin walikuwa kwenye mchakato wa kuchapisha kitabu cha On the Other Hand. Walimpatia nafasi Geoff Bridgford ya kuwa moiga ngoma rasmi wa bendi, Bridgford mwanzo alifanya kazi na bendi ya The Groove pamoja na Tin Tin.
1970 albamu ya 2 Years On iliachiwa mwezi Oktoba huko Marekani na mwezi wa Novemba kwa upande wa Uingereza, nyimbo bora katika albamu hiyo ilikuwa ni "Lonely Days" ambayo ilishika nafasi ya tatu kwa upande wa Marekani, kazi kubwa ilifanyika katika kuitangaza albamu hii, walizuru kwenye vipindi mbalimbali vya luninga kama vile, The Johnny Cash Show, J ohnny Carson's Tonight Show, The Andy Williams Show, The Dick Cavett Show pamoja na kipindi cha The Ed Sullivan Show.
Albamu yao ya tisa ikawa ni Trafalgar ambayo iliachiwa mwishoni mwa 1971 huku wimbo wa "How Can You Mend a Broken Heart" ukisumbua sana Marekani kwa kufika nafasi ya kwanza huku wimbo wa Israel ukifika namba mbili kwa upande wa Uholanzi. Wimbo wa "How Can You Mend a Broken Heart" uliwapatia nafasi ya kipekee sana bendi Ya The Bee Gees ya kuingia kwenye tunzo za Grammy kwenye kipengele cha Best Pop Performance by a Duo or Group with Vocals.
1972 walitikisa tena Marekani kwa nyimbo yao ya "My World" kwa kufika namba 16, mwaka huo huo wimbo wao wa "Run to Me" uliwarudisha rasmi kwenye chart ya nyimbo 10 bora za Uingereza ikiwa ni baada ya miaka mitatu ya kupoteana. Bridgford aliondoka kwenye bendi kutafuta changamoto sehemu nyingine na bendi ikabakia na watu watatu, Barry, Robin pamoja na Maurice. Novemba 24 1972 wakawasha moto kwenye tamasha la "Woodstock of the West" pale Los Angeles Coliseum walifanya maajabu makubwa sana wakiwa pamoja na Sly and the Family Stone, Stevie Wonder pamoja na bendi matata sana ya the Eagles. Mwaka huo waliimba wimbo wa "Hey Jude" wakishirikiana na Wilson Pickett.
1973 kwa mara nyingine the Bee Gees wakaanza kupoteza mvuto kwa mashabiki, albamu yao ya Life in a Tin Can ambayo iliachia chini ya record label mpya ya RSO Records ilifanya vibaya, albamu ambayo ilikuwa na nyimbo kama vile "Saw a New Morning", ambayo hii ilishika namba 94, namba ya chini zaidi kuwahi kushikwa kwa wimbo kutoka the Bee Gees. Baadaye walijipanga na kutoa albamu nyingine ila bado hali ilikuwa mbaya, mwaka 1973 walishirikia na wasanii kadhaa, "Money (That's What I Want)" waliyoimba pamoja na Jerry Lee Lewis pamoja na wimbo wa "Reelin' and Rockin'" walipoimba"Johnny B. Goode".
Baada ya ziara yao Marekani mwanzoni mwa mwaka 1974 pamoja na ziara nyingine huko Canada, bendi ilianza kufanya maonyesho yao kwenye kumbi ndogo, Barry akakaririwa akisema kuwa iliwabidi kujishusha ili wapate chochote kitu kutoka kwa watu. Stigwood aliwasaidia sana kwani alikutana na Ahmet Ertegun ambaye alikuwa ndo mkurugenzi wa Atlantic records upande wa Marekani, hivyo waliandaliwa nafasi ya kwenda kufanya nyimbo pamoja na mzalishaji nguli wakati huo, Bwana Arif Mardin, walitengeneza nyimbo kama vile, Mr. Natural ila bado hali haikuwa nzuri kwao hata kidogo.
Baada ya kujaribu kila funguo kufungua mlango na bado ngoma ikabaki ngumu, Mardin aliwapatia wazo moja, aliwaambia wajaribu kubadilisha aina ya muziki na kufanya muziki wa miondoko ya Soul, basi wakaanda onyesho mubashara na kumtafuta Alan Kendall kucheza vyema na gitaa, Dennis Bryon upande wa ngoma pamoja na Blue Weaver fundi wa kucheza na kinanda na hii ndo ikawa combination hatari ya bendi ya The Bee Gees.
Eric Clapton aliona jahazi la The Bee Gees linaanza kuzama hivyo aliwapatia wazo kaka hawa kuwa wahame na waende Miami, Florida wapate kurekodi nyimbo zao pale Criteria Studios, na walipata msaada mkubwa wa mawazo kutoka kwa Mardin pamoja na Stigwood kuwa wabadilishe aina ya muziki ili kuteka tena soko. Mawe mawili makubwa yakapikwa na kupikika vyema, hapa ni "Jive Talkin'" ambayo ilishika nafasi ya kwanza kwenye chart za Marekani, pamoja na jiwe la "Nights on Broadway" ambayo ilishika namba saba, ukisikiliza mdundo na ala ya muziki wa sasa ni kama walifahamu sehemu ya kupiga deals, mashabiki wakaanza tena kufuatilia ambacho kinafanywa na The Bee Gees. Kuingiza nyimbo mbili kwenye chart za Marekani, "Jive Talkin" pamoja na "Nights on Broadway" ikawa ni mara ya kwanza kwa The Bee Gees kuwa na nyimbo zaidi ya moja kwenye chart za Marekani huku Main Course ikiwa ndo albamu pendwa ya R&B.

Mwisho wa sehemu ya kwanza tukutane sehemu ya pili na ya mwisho!