The Big Result Now, Mwanafunzi Asiyeweza Kuandika Jina Lake Afaulu Darasa la Saba

1954tanu

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
1,038
Reaction score
487
Mfumo na mkakati wa kuongeza idadi ya wanafunzi ili kujaza madarasa katika shule za sekondari; mfumo ambao unashadidiwa na kile kinachoitwa "BRN" imeanza mapema kuonekana. Matokeo ya darasa la saba mwaka huu 2013 yametoka na miongoni mwao ni kijana ambaye uwezo wake wa kuandika jina lake ni mdogo mno. Hata hivyo, kijana huyo amekuwa mmoja wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani 2014.
 
This is amazing grace. Huu mpango inawezekana ukawa mzuri lakini ulianza bila mikakati madhubuti. Kwa msingi huo unaweza kuzaa BSN- Big Shame Now.
 
Hakuna cha ajabu hapo kama maswali yote ya mtihani wa darasa la saba ni kuchagua hata akifumba macho akipiga kwenye kibox chochote ndiyo jibu, si atafaulu na bado mtaona maajabu mengi.
 
sema vizuri ni wapi huko? Toa detail vema jf we dare to talk freely
 

kwa mtu anayejua kama kuna mtoto yeyote wa waziri, katibu mkuu hata mkuu wa wilaya anayesomea shule za msingi za sisi walala hoi atuwekee hapa jamvini tafadhari! Hiki kitakuwa kioo cha wengi!!
 
Hii ni aibu Kama taifa. Tumepoteza direction. Hizi Quick fixes za serikali hazitusaidii bali kutuangamiza kabisa Kama taifa!
 
bahati nzuro mfumo wetu pendwa umehakikisha no division zero!

div_zero_probability=0;
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…