Ukiongelea matajiri wengi wa Tanzania ambao wamepata utajiri wao kutokana na imani za USHIRIKINA kama ndugu zangu WAKINGA wa IRINGA ambao wako Kariakoo, Mbeya au Tunduma ambao wamepata utajiri wao kutokana na imani za kishirikina ni sawa, hawa watu hawahitaji elimu, ingawaje anaweza kuwa Vipanga, hata kama hawajasoma, kwani IQ inategemea unaipima kwa nini! , watu hawa wao imani yao ndio mtaji wao, na imani hiyo ndio inawaletea mafanikio. Vilevile, vipanga wengi hawapendi kujiajiri wao hupenda kuajiriwa ili walipwe mshahara na hao wajasiliamari.
Kama anasoma vitabu vya akina Robert Kiyosaki, vyenyewe ndio vinasema hivyo, Ili uwe TAJIRI huhitaji kufahamu mambo mengi ya formal schools ila unahitaji kufahamu masuala ya Biashara, mfano uwe na Financial inteligency, management skills kwani vitu kama hivi havifundishwi kwenye mashule yetu na ili uvipate unahitaji kukaa na watu wanaovifahamu au kufanya kazi nao ujifunze. Kufahamu haya huhitaji kuwa kipanga, ila inahitaji tu kuwa na imani au uthubutu wa kuwa inawezekana (GUTs).