Uchaguzi 2020 The Blue Family waache utoto na kutumika, wakisimama wenyewe wanaweza

Uchaguzi 2020 The Blue Family waache utoto na kutumika, wakisimama wenyewe wanaweza

X-bar

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Posts
1,006
Reaction score
1,156
Inapotokea mtifuano ndani ya chama, wana CCM ambao hawaridhishwi na maamuzi fulani ya chama chao, hawako tayari kujenga nguvu ya kuipinga CCM kwa kuungana na vyama makini na vikongwe vya upinzani; hii ndo itikadi ya wana CCM. Ninaposema vyama makini na vikongwe vya upinzani namaanisha CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi ( The Blue Family), vyamba ambavyo kila kimoja kwa wakati wake viliichachafya CCM katika chaguzi zilizofanyika na vikawa vyama vikuu vya upinzani.

Kutokana na msukumo wa itikadi za kidini, baadhi ya wana CCM hawakuridhishwa na uongozi wa Rais Kikwete kwa kuleta mifumo serikalini inayogawa "fursa sawa" kwa raia wa dini zote kwenye elimu, ajira na masuala mengine kama vile OIC na mahakama ya kadhi. Hivyo basi, kuelekea uchaguzi wa 2010 wana CCM hao walidhamiria kuipasua CCM ya JK kwa kuunda CCK (CCJ?) chama ambacho kwa bahati mbaya au nzuri kiliishia "pre-mature death" kutokana na mbinu za kisiasa za JK dhidi ya chama hicho

Kifo cha mapema cha chama hiki kipya haikuwa ndo mwisho wa agenda dhidi ya JK. Jamii isiyompenda JK iliwaona wale wana CCM ambao waliaminika wangemtenza nguvu JK kuwa ni wasaliti kwa kushindwa kujitenga naye. Hivyo basi, iliwabidi watafute chama kingine miongoni mwa vile makini vya upinzani vilivyopo ili kuendeleza agenda dhidi ya JK.

Waliamua kuwa Chama ambacho kingefaa ni CHADEMA kwa kumtumia Dr. Slaa kutekeleza agenda hiyo. Ni muhimu kukumbuka kuwa kuelekea uchaguzi wa 2010 CHADEMA haikuwa na mtu ambaye angegombea nafasi ya urais kwani Mbowe ambaye aliwahi kujaribu katika uchaguzi wa 2000 alijiona kuwa hatoshi katika nafasi hiyo ya juu bali aendelee na ubunge.

Ndipo iliwalazimu kumshawishi Dr. Slaa kwa kumhakikishia "background support" ya jamii isiyompenda JK na hatimaye Slaa alikubali kugombea katika dakika za lala sama lakini kwa masharti/mkataba maalumu wa kufidia maslahi yake ambayo angeyapoteza kwa kuukosa ubunge na urais. Dr. Slaa aiingia vitani na huu ndo msingi wa CHADEMA kupata nguvu na kuipiku CUF kwenye nafasi ya chama kikuu cha upinzani.

Unaweza kujiuliza kwanini agenda dhidi ya JK ilitekelezwa kupitia CHADEMA badala ya CUF au NCCR. Jibu ni kwamba CHADEMA wakati huo bado kilikuwa "underground" ukilinganisha na vyama hivi viwili ambavyo viliweza kushika nafasi ya chama kikuu cha upinzani. Kwa maana nyingine ni kwamba wana CCM walihisi isingeweza kuambikiza na kukubalika itikadi yao ya asili kwenye vyama vyenye itikadi thabiti. Wanaona ni heri kuteka vyama vidogo au kuanzisha vipya ambavyo wanaweza kuviambukiza itakidi ya "u-ccm" bila vikwazo. Hoja hiibinaendana na kauli ya Mbunge Bwege aliyesema ameamua kuhamka ACT badala ya CHADEMA au NCCR kwasababu chama hicho bado kichangaza na hivyo ni rahisi kukifinyanga kwa namna uitakayo kitu ambacho vi vigumu kwa chama kikongwe.

Tulipoingia uchaguzi wa 2015, wana CCM waliohisi wangekatwa kwenye chama hicho waliamua kuunda chama kipya, ACT-Wazalendo, ili kiwe kimbilio lao. Kuna kadi za uwanachama wa chama hicho ambazo zilihifadhiwa kwa ajili ya vigogo ambao wangeamia kugoka CCM. Moja wapo ya kadi hizo ni Kadi No. 1 aliyokabidhiwa Maalim Seif.

Kutokana na hofu ya CHADEMA kuwa ingezidiwa nguvu/umaarufu ambao ACT ingepata kutoka kwa wana CCM waliotaka kukimbilia huko, chama hiko kiliona hakina namna zaidi ya kuwavutia wana CCM hao waingie kwenye chama hicho kwa kuwapa zawadi ya nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho hata kwa gharama ya makada wenyeji na wna UKAWA wengine. Ndipo Lowassa na wafuasi wake toka CCM wakakata kona na kuingia CHADEMA badala ya chama chao walichokiandaa. Hii iliwezakana kwavile tu CHADEMA yenyewe ilikubali tena "kufinyangwa" na kutumima na wana CCM hao kitu ambacho Lowassa mwenhewe hakuamini inbekuwa rahisi hivyo.

Hasira za mtifuano katiaka uchaguzi wa 2015 kwa upande wa Lowassa na wafuasi wake ziliisha kwa wao kurejea itikadi yao ya asili, CCM. Tunapoingia uchaguzi wa 2020, mambo ni yale yale; kuna mtifuano ndani ya CCM na safari hii ni zamu ya Benard Membe. Membe yeye hajajiunga na "The Blue Family", amekimbilia ACT (Mneya City).

Swali la kujiuliza hapa ni kwanini BM hakwenda CHADEMA , CUF wala NCCR. Swali hili linajibika kwa hoja nilizotaja hapo juu.

Kwanza, kama nilivyosema, ACT ni "banda" la wana CCM na mlango wake uko wazi kwa mwana CCM kuingia bila hodi.

Pili, ACT ni chama ambacho bado kipo "underground" na kutokana na uduni kiko tayari kupokea, kufinyangwa, kuendeshwa na kutumika na wakimbizi waliolelewa kwa itikadi za CCM.

Tatu, wa ACT kuendeshwa na BM ni neema kwao kwa kuwa wanaona ndo fursa ya kujenga umaarufu wa chama kwa kuwa na mgombea katika nafasi ya urais.

Nne, BM mwenyewe anahisi hasingepewa fursa ya kugombea urais katika "The Blue Family" kama ilivyokuwa kwa mwenzie Lowassa kutokana na vyama hivyo kujifunza kuwa wana CCM si watu wa kuaminika kuwapa nafasi muhimu upinzani. Zaidi ni kwamba, vyama hivyo tayari vina watu wake ambao wamedhamoria kwa dhati kusimama katika nafasi anayoitaka BM.

Jambo la muhimu kwa The Blue Family ni kuacha "utoto" na kushambuliana wenyewe kwa wenyewe. Vyamaa hivi vinapaswa kushikamana kuacha kukubali kutumika na wakimbizi wa CCM. Wakishindwa kuungana basi wasimame wao kama wenyewe.

Zaidi wanatakiwa wawasome na kuwaelewa Zitto Kabwe na Maalim Seif. Wajiulize maswali haya.

1. Kwanini Maalim Seif alikimbilia ACT badala ya CHADEMA walilmkaribisha kwa mikononmiwili. KwanininI hakujiunga na NCCR?

2. Kwanini BM hakujiunga na CUF chama chenye ngome yake mikoa ya kusini ambako ndo asilinya BM? Kwanini BM atamani wanamageuzi wa Lindi na Mtwara wakifanya harakati kwenhe chama kipya cha ACT badala ya CUF?

3. BM anapolilia muungano wa vyama vya upinzani, je yuko tayari kukaa pembeni na kumpisha Lisu Nyalandu au Lipumba kwenye kugombea nafasi y aurais?

4. Kwanini ZZK anajikita kueneza ACT Lindi na Mtwara mikoa ambayo angalau kuna watu wenye itikadi za mageuzi ukilinganisha na Dodoma, Pwani au Rukwa?
 
CUF ilishakufa kusini haina nguvu tena, nguvu hii imehamia ACT kusini, Lipumba ameimaliza CUF na wale waliokuwa CUF msimamo wote wamehamia ACT....
 
Back
Top Bottom