The dark side of business

#uko sahihi kabisa_wanaobishana naww wao ndo hawana akili
Mimi sibishani.

Ila najenga hoja kwamba,

Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina kwa nini mtu asiutumie kwa nguvu zake zote awazidi au angalau basi awafikie matajiri wakubwa duniani kama kina Elon musk, Jeff Bezos, Warren Buffett?

Toa kafara za kutosha ikiwezekana hata ukoo wako mzima kama kweli utaweza hata kumzidi Elon musk, na kama kweli kuna utajiri wa kishetani.
 
#hoja kama hio majibu yake nimarefu sana
 
#hoja kama hio majibu yake nimarefu sana
Sio marefu kama kweli kuna utajiri wa kishetani ile orodha ya Forbes waafrika wangejazana pale.

Tajiri wa Afrika alikuwa ni Mansa Musa tu.

Hawa matajiri wa kiafrika wanaojidai kuna utajiri wa kishetani ni makapuku tu wanalishana matango pori, wala hawana kitu.

Ukidai kuna utajiri wa kishetani utumie kwa nguvu zako zote walau basi uwe kama Dangote.
 
Awapo Kwa 7bu ata hyo dark side Ili uwe juu zaid inahtaj talent na creativity Ili uongeze kipato Kwa sababu wao wanakupa mvuto wa wateja au wafuasi lakn pia itahtaj talent yako au elimu na creativity yako Ili kukua zaidi most of Africans they engeged on it but they have poor creativity and IQ
 
Hizo ni taratibu za wachina za ibada,

Wana imani zao zilizo tofauti na zetu.
Hakuna tofauti broo,
Ibada kama hizo ni asili yao kama ambavyo ibada za aina hiyo ndiyo asili kwa Waafrika.

Au ulifikiri hizo ibada za dini za kuletewa na Wazungu na Waarabu ndiyo asili ya Waafrika?

Kwa taarifa yako hizo dini za kuletewa hata China zipo
 
Ni ile stage magic ya kufurahisha watu, ya kisanii, mnaita mazingaombwe...
Hapo wanaongelea magic and witchcraft, kwa hiyo uchawi umo.
Uchawi tunaoongelea hapa, wa kukupa utajiri, kufanya matatizo yako yatoweke, haupo ndugu...
Haupo wapi?
Mimi siyo mfuasi wa uchawi, ila naamini kuwa uchawi upo na kuna namna unawasaidia baadhi ya waumini wake.

Em msikilize huyu gwiji hapa chini anavyotoa ushuhuda wa kupata mpunga mrefu kupitia mambo hayo..

View: https://youtu.be/e4InVI3bOGQ?si=JjKosqkSNm6vHdGq
 
Maisha bwana yana siri nyingi sana za ajabu,baada ya kipindi kirefu kupotezana na mshikaji wangu nilisoma nae o-level.Tukakutana mjini kwenye pirika za hap na pale

Tukapiga story nyingi kipindi hicho mimi nilipata matatizo kazini yalitokana na husuda na vijicho na fitina nyingi sana nakawa nimesimamishwa kazi.Basi kwenye story jamaa akanieleza anayopitia kwenye company ya Waasia ,jamaa alikuwa anafanya sales vizuri sana mpaka jamaa wakawa wanamkubali

Picha likaanza walimwambia ukifanya vizuri zaidi kuna bonus tutakuwa tunakupatia,jamaa ndani ya mwaka akapata bonus kama ya 12m kosa likaja kwenye kudai bonus yake,jamaa hawakumpa wakaanza kumzingua .Mshikaji akaanza kuugua sana nenda sana hospital wapi,akaenda upande wa pili kwenye maombi/dua akaanza kuona kidogo uelekeo.

Jamaa alivimba sana mguu ,kuanguka sana ofisini alikua na maji yake ameyasomea alienda nayo job ile amemwagia kile kiti chake alipigwa mweleka mkali sana chini.
Naskia jamaa walitaka kuchukua nyota yake na wamfute kwenye sura ya dunia.Jamaa kwenye kupambana atafute kazi sehemu ,zimetokea offer nzuri 2 with mega salary lakini zinayeyuka mwishoni.Kuna moja alishaongea kabisa na jamaa wakamwambia tafuta leseni tutakupa gari kwa ajili ya kazi baada ya makubaliano kilakitu.J3 anajiandaa kwa ajili ya kwenda kusaini mtoto wake wikiendi aliumwa sana hali chochote ,hospitali hakuna ugonjwa siku za kurepot kashindwa kwenda kazini
Story huwa ni ndefu sana ya huyu mwanangu.Lakini sasa hivi jamaa kutokana na changamoto hizo amekua mtaalamu wa dua ,imebidi ageukie upande wa Mungu kufanya maombi sana ,jamaa huwa halali kabisa anasali sana.
 
Binafsi nilishawahi kufanya biashara namuelewa sana mtoa story. Hakuna kitu kinampa stress mfanyabiashara kama biashara ilikuwa inafanya vizuri halafu ghafla ikaanza kufilisika.

Anasema kwa niaba ya wengi huku.
ndio situation niliyonayo sasa hivi..mishale ni kibao nimemwelewa ila ujasiri wa kwenda upande wa pili ndio shida...
 
Kwani wewe una uhakika Gani uliowataja hawatoi kafara
 
Haujajibu maswali yangu mkuu, rudia kusoma unijibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…