The dark side of business

Kwani wewe una uhakika Gani uliowataja hawatoi kafara
Kafara za nini?

Wanyama, binadamu, au kafara za aina gani?

Kama kutoa kafara ndio ingekuwa inafanya utajiri kuongezeka, Basi Elon musk ndio angekuwa mtoa kafara namba moja duniani.

Lakini sivyo, Kuna wakati Elon musk utajiri wake hushuka na si kwamba eti hajatoa kafara ndio maana utajiri umeshuka hapana, Ni kwa sababu hisa zake, uzalishaji wake umepungua kwa kiasi fulani ndio maana anapitwa na wengine.

Hakuna shetani anayetoa utajiri.
 
Tupo Nyuma Yako Mkuu
 
EPISODE 10
Ilipoishia...

Baada ya miezi 3
Ngurumo alinitafuta
"Vipi kijana mambo yanaendeleaje?"
Mm:isee mambo ni 🔥🔥kuna zawadi nitakupa mzee wangu!
Ngurumo:sawa ila wewe endelea kufata masharti utafika mbali Sana....una nyota kali sana ya biashara lakini ni muhimu kujua wale ng'ombe wawili wanamaanisha nini?kisha akakata simu..
Niliitafakari hii kauli ya mzee ngurumo sikupata jibu..........

Sasa tuendelee
Ile kauli ya ngurumo ilinipa kutafakari kwasababu huyu mzee akiongea kitu huwa anamaanisha(nilijiuliza mwenyewe,wale ng'ombe Wanamaanisha nini? Sikupata jibu.

Niliendelea na biashara kama kawaida,mtaji ulikua kwa kasi,kwasababu 70%ya faida niliirudishia kwenye mtaji,ofisi zote mbili zilikuwa na nyomi ya wateja,tulipiga kazi mpaka mwaka unaisha working capital inasoma 250M,mwaka wa pili wembe ulikuwa ulele ila mwishoni mwa mwaka wa pili mambo yakaanza kuslow down!

Nikakumbuka ile kauli ya ngurumo kuhusu wale ng'ombe,nikahisi itakuwa Kuna uhusiano na hiki kinachonitokea,ikabidi nitafute namna ya kufungua hiyo code!

Niliwaza huenda bijan atanifungulia hii code,maana wale viumbe wana IQ kubwa Mara kumi ya mwanadamu.

Nikafika home,nikazama chumbani kama kawaida,niliita bijan....kimya,nikaita tena bijan...ukimya ulitawala,nilikaa mule chumbani najiuliza nini kinatokea mbona sio kawaida, baadaye kidogo bijan alitokea,nilimuuliza"kulikoni"lakini hakunijibu,alikaa kimya na baadaye kidogo alitoweka,nilipoona bijan hasomeki,nilipata wazo la kumtafuta mzee fabi,maana nilikosa kabisa utulivu wa kiakili....

Mm:habari,shikamoo mzee wangu

Mzee fabi:marahaba kijana, unaendeleaje?vp changamoto zako zimeisha?

Mm:aha wapi!mzee wangu,biashara hazihishiwi changamoto,linatoka hili linakuja hili(nilimuuliza mzee fabi kuhusu ng'ombe kiroho wana maanisha nn?)
Mz fabi:kwanini umeniuliza swali Kama hilo?
Mm:mzee nimeota ndoto,kwenye ndoto nikaona ng'ombe wawili,baada ya hapo biashara zikaanza kusua sua(ilibidi nimdanganye mzee fabi,asije akanishtukia Kama nimejiingiza kwenye dark side)

Mz fabi:mmh,kijana suala la ng'ombe kwny ulimwengu wa roho ni fumbo gumu...nakumbuka uliwahi kuniambia wazazi wako waote,walishafariki?(uliuliza mzee fabi)
Mm:ndio,walifariki tangu niko sekondari.
Mz fabi:na kwenu mlizaliwa wangapi?

Mm:tumezaliwa watatu,Mimi ndio firstborn na nina wadogo zangu wawili,mmoja wa kike na mwingine wa kiume.

Mz fabi:kijana sijui imani yako,lakini ng'ombe kwenye ulimwengu wa roho wana maana mbili,
1)ng'ombe humaanisha mwaka yaani kipindi cha miezi 12,kwahiyo Kama uliona ng'ombe wawili.maana yake ni miaka miwili....
"Nilikuwa makini sana kumsikiliza mzee fabi,huku nikilinganisha na situation yangu"

..kabla mzee fapi hajamalizia...alitokea bijan akasimama mbele yangu,alionekana ni mwenye hasira.
Bijan:huyo mzee ni mtu mbaya sana,achana naye,rafiki zako wa ukweli ni sisi na ngurumo.

Wakati namsikiliza bijan,mzee fabi aliendelea kuita halo...haloo,ilibidi nimwambie,samahani mzee wangu nitakutafuta baadaye.

Wakati naendelea kuongea na bijan,simu yangu iliita,kucheki ni mzee ngurumo.

Ngurumo:kijana naona umeanza kuvunja masharti,?

Mm:mbona sijavunja sharti lolote!
Ngurumo:huyo mzee ulikuwa unaongea naye nini?
Mm:ni mambo ya kawaida tu
Ngurumo:sawa,sasa naomba wewe na bijan mje kwangu leo saa mbili usiku kuna mambo tuyaweke sawa.

Baada ya kuachana na bijan, niliwaza kuhusu ile tafasiri ya mzee fabi kwamba wale ng'ombe wawili ni miaka miwili,niliona tafasiri yake ina ukweli,kwasababu miaka miwili imeisha tu mapichapicha yanaanza tena.

Nyumbani kwa ngurumo
Ilipofika saa mbili kimili,Mimi na bijan tulikuwa tumeshafika nyumbani kwa ngurumo.

Ngurumo: nimewaita ili tuimarishe agano, miaka miwili imeshakwisha na mafanikio tumeyaona,sasa ni wakati wa kukuinua uwe mfanyabiashara mkubwa Tanzania yote wakujue..

Mm:nakuamini sana mzee wangu,kila unachosema kinatimia,ni ndoto yangu niwe mfanyabiashara mkubwa sana hapa tanzania.

Ngurumo:usijali,hicho ni kitu kidogo sana kwangu(ngurumo aliingea huku akijipiga kifua)

Aliendelea kuongea...........
Ngurumo:sasa inabidi utoe ng'ombe wawili tena
Mm:haina shida,niko tayari hata kesho...
Ngurumo:kesho na kesho kutwa kuna mambo inabidi tuyaweke sawa,siku ya tatu ndio tutawatoa hao ng'ombe(ngurumo alimaliza kuongea)

Kesho yake
Nilipoamka asubuhi, kucheki simu yangu nakuta text ya mdogo wangu wa kike,ananiambia kuna ndoto ameota kuhusu mimi!nilishtuka sana, kwasababu huyu mdogo wangu akiota kitu basi 100% ni kweli.
"Bro nimeota usiku wa kuamkia leo,mimi na mdogo wetu wa mwisho umetutoa kafara"(hiyo text ilisomeka hivyo)

Wadau,kwenye ulimwengu wa roho,kuna kitu kinaitwa "binah"hii ni kama spiritual intelligence ambayo inamsaidia mtu kujua hatari iliyopo mbele hata kabla haijatokea,binah wanayo sana wasichana bikra na wanawake wanao mcha M-ngu(mwanamke akizini anapoteza vitu viwili "binah na loyalty" hii ndio sababu gadafi alikuwa na mabodigadi wa kike ambao ni bikra,alilenga binah na loyalty)

Tuendelee na ile sms
Baada ya kusoma ile meseji,nikamjibu
"Hiyo ni ndoto tu mdogo wangu,ipuuze,siwezi kufanya hivyo"
akanitumia text tena
" Mimi nikiotaga huwa inakuwa kweli,kama una mambo yako naomba uachane nayo"
nikamjibu
"Mimi ni mtu poa sana sina baya na nyie wadogo zangu ninawapenda,siwezi fanya lolote baya"
akamalizia kwa kunijibu"mh haya"
hii siku nzima nilishindwa kufanya chochote,nilikaa tu kitandani nawaza hiki alichoniambia mdogo wangu,nilivuta picha kwamba hao ng'ombe wawili ndio hao wadogo zangu,ndio maana hata mzee fabi aliniuliza nina wadogo wangapi?..nilijilaza pale kitandani,mpk nikapitiwa na usingizi....

kesho yake
Ikawa imebaki siku moja ya kuwatoa wale ng'ombe,akili yangu ilibadilika,niliwaza mbona ng'ombe wa kwanza niliwatoa na hakukuwa na baya,nikawa najitia moyo kuwa hawa watakuwa ni ng'ombe tu wa kawaida kama wale wa mwanzo..wakati naendelea kutafakari nilikumbuka mzee wangu(baba mzazi) akiwa amelazwa anakaribia kukata moto,aliniambia"wewe ndio mkubwa,unajukumu la kuwaangalia wadogo zako"haya maneno ya mzee wangu yalinifanya niwe njia panda,sijui niwatoe hao ng'ombe au niache? Nikiacha lazima mambo yangu yataharibika na nitapatwa na majanga lakini pia nikiwatoa harafu ndio iwe kweli ni wadogo zangu,nitapata laana ya mzee,kumwaga damu isiyo na hatia....
**********************************
Siwezi kukaa njia panda daima lazima mwisho wa siku nifanye maamuzi,bado siku moja...je nitachukuwa maamuzi gani?............khodahafez
 
Leo weka hata ep. Mbili mkuu
 
Mzigo umekaa poa sana, ila kumbuka ulisema ijumaa hii unashusha wote.
 
Ngo'mbe kama Ngo'mbe
 
Noma sana!
 
Tanzania Drea
Vp mkuu hali yake imabadirika? Maisha yake yameboreka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…