The dark side of st joseph college of engineering & technology

brainee

Member
Joined
Dec 6, 2010
Posts
24
Reaction score
3
1.Asilimia zaidi ya tisini ya Lecturers ni Wahindi toka Tamil Nadu na hakuna Professor wala PhD holder hata mmoja chuo kizima

2.Dress Code:Round colar Tshirts for men haziruhusiwi,sleeveless shirts for girls not permitted

3.Ni Chuo cha elimu ya juu pekee kinachotumia kengele kumeneji muda !!

4.Attendace:kwenye Kila kipindi Lecturer huita majina na wanachuo hawa huwajibika kuitika "present"

5.Huruhusiwi kuingia kwenye kipindi baada ya kengele kugonga..

6.Mwanachuo hulipia fedha ya mtihani(UE) kila semester including supplementary exams ambayo kila mmoja ni sh.7500(kwa kawaida kila semester ina subjects 6)kumbuka hii ni mbali kabisa na Ada

7.Kila mwaka wa masomo mwanachuo hutakiwa kulipa shilingi laki moja(100,000) kwa ajili ya stationary.Stationary zenyewe ni counter books 6 na notebooks zingine mbili kwa ajili ya lab works (per semester).Vilevile hii ni nje kabisa ya tuition fee

8.Masomo huanza saa mbili mpaka saa kumi..break kwa ujumla ni saa moja na nusu!!

9.Jambo jingine muhimu ni kuwa lecturers wana uWezo wa hali ya chini sana ambao ni miujiza kusema sentesi mbili sahihi za kiingereza

****************MNAKARIBISWA NYOTE************
 
Serikali itaifanyia kazi mwongozo wako ila ni vizuri ungetoa ushauri kwa serikali huo uongozi wa hicho chuo na malecture wao tuwapeleke mwabepande au
 
mmmh!...uzuri wa bodi si ubora wa engine,chuo kina jina kubwa kumbe ndani uozo,bado ktk engineering hakuna mpinzani wa DIT,poleni sana
 
puuuuuuu! msiwe wavivu nyie,

Pili, walimu hawana tatizo,

wanafunzi, wa TZ wacheni uvivu
 
dooooo!!!! kaazi kwelikweli!!!
 
Sitaki nikuamini unachokisema, ila what i know ni kwamba kuna ma prof huwa wanatoka CoET mfano mzuri ni prof john yule jamaa wa Thermal dynamic pale energy department kama bado ipo manake ni siku nyingi zimepita. kitu kingine ni kwamba jamaa wanahaki ya kuwatoza hela ya sup kwani hamstahili kupata sup kwa mitihani mnayotungiwa, prof John alikuwa anawakomoa sana vijana wa mwaka wa pili MECHE by then lakini ukiona mitihani ya chuo chenu ilikuwa rahisi mno.
 
Dah me nlikuta mahal wanafunzi from hii chuo wanafanyiwa interview,,eventhough jamaa ana GPA ya 4.2 aliulizwa betri ya gari ina volts ngapi akasema 240V kupewa engine afungue na kirudishia ndo hata kuifungua alishndwa and yupo serious kbsa na kamaliza bachelor hapoo
 

Alikua kasomea degree ipi???
 

Duh!Kuna haja ya mainjinia wakimalimaliza degree zao,wapitie VETA angalau miezi 6!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…