Mzunguko wa tano wa kombe la FA kuanza hii leo ambapo Burnley atakuwa nyumbani akiikaribisha Bournemouth huku Manchester United akimenyana na West ham United.
Baada ya kuwachakaza Majogoo wa London bao 4-1 katika Dimba la Anfield tarehe 7 katika mchezo wa ligi kuu England, Manchester city atakutana na Swansea city ambaye atakuwa nyumbani Jumatano Februari 10.
Michezo mingine ya Kombe hilo ambayo itachezwa siku hiyo ni kati ya Leicester city dhidi ya Brighton huku Everton akiwa nyumbani akiikaribisha Tottenham Hotspur.
Na Alhamis tarehe 11, Wolves atavaana na Southampton huku Barnsley akimenyana na Chelsea.