Kutambua vyeti vya diploma inategemea sana level ya syllubus husika ili-cover nini na kw amuda gani..............na ili ujiunge na kozi fulani kuna minimum requirements zake........sio ili mradi inaitwa diploma.............
Hii ina apply kwenye vyuo vingi vya kueleweka.
Diploma ya Imperial College ni "moto"..........pamoja na kutambulika kuwa ni sawa na Bachelor degree.....still watu hujitambilisha kuwa ni holders wa Dip Imperial College...........
Nyumbani enzi zile...........ni waliofaulu tu ndio walikwenda shule za serikali na kujiunga Chuo Kikuu DSM ilikuwa lazima ufaulu A'Level...........average performers (not to disrespect anybody) wengi waliishia Ardhi (ukiondoa Architecture course), Mzumbe, Chuo cha Ushirika nk nk...............kuna watu (average performers) walipitia hizo colleges na wakabadilika kuwa VIPANGA kweli kweli.............LAKINI bado wana aina fulani ya "Ntimanyongo" kwa wale walioingia UDSM na chuo chenyewe...........huu ndio ukweli.
Binafsi sikupata bahati ya kuingia pale UDSM.......lakini ninakiheshimu kile chuo.......nalikuwa najivunia kuwa tuna Chuo maridhawa.....recently kimeanza kuporomoka "quality"...........kwa kweli inasikitisha.......na huu sio wakati wa kukibeza.........ila wanaowajibika nacho inabidi wachukue hatua ili kurudisha hadhi yake............Prof Mukandara unatakiwa ujenge hoja chuo kirudi kwenye hadhi yake
Prof Mukandara
Ni upuuzi kusema eti keki kubwa wanapewa UDOM...............unatakiwa upunguze matumizi ambayo ni un-necessary............hivi ukitumia saloon car (4 cylinders) kile kibao pale Hill kuonyesha kuwa hayo ni makazi yako kitaondolewa?..........au u-VC utakuvuka?....anzisha policy za kubana matumizi by offsetting un-necessary cost kwa mambo muhimu tu..............
Matatizo ya UDSM ni compounded lakini pia siasa ndiyo imeifikisha UDSM pale ilipo, ilipoanza mikakati ya kuongeza rundo la wanafunzi bila kufanya expansion ya any required facilities. Ikaja ishu ya upendeleo kwa wanawake kuleta usawa sort off, let them go hata wasipokidhi requirements.
Pia aina ya walimu wa UDSM walio wengi unakuta hakuwahi kufanyia kazi kile anachofundisha. Mtu mwenye GPA kali basi automatically anabakishwa chuo anaendelea kusoma Masters, then PhD mfululizo baadae anaanza kufundisha. Anafundisha vitu ambavyo hata yeye mwenyewe hazifahamu vizuri hands on challenges zake. Zaidi zaidi ni akademiksi tu.
Kingine pia ni aina ya wanafunzi, wengi wao wakiwa na misingi mibovu. Ufaulu wa kutumia past papers, madesa na wizi wa mitihani. Huwezi kuamini mtu mpaka anafika chuo kikuu anaweza kuwa hajawahi kutumia vitabu ili kuelewa kwa mapana kile anachofundishwa.
Serikali kutokutilia maanani na kuona UDSM is just an expense. Ukiangalia the case mfano ya pale Engineering baada tu ya wajerumani kukata funding, mwishoni miaka ya tisini basi ikawa ndiyo kama mwisho wa kwenda mbele. Serikali haikufanya compensation badala yake ikazidi tu kuongeza wanafunzi.
Ukija kwenye suala zima la research, ntatolea mfano uhandisi. Research nyingi zilitakiwa kuendeshwa na industries kwa sababu is easy kupata funding kama utafiti huo utaisaidia hiyo industry. Lakinni hatuna viwanda na vingi vilivyopo ni magumashi magumashi. Ukienda karibu kila kiwanda kuna matatizo yamekuwapo hapo for ages na yanahitaji utatuzi. Ndiyo maana utakuta nchi kama South Africa iko mbele labla mara 1000 zaidi ya nchi nyingi za kiafrica. Sasa sisi research zetu hata zile za kuboresha majiko ya mkaa tunategemea msaada kutoka SIDA, usaid, VSO etc. Research institutes kama vile TIRDO nadhani ilishajifia nazo ni mwendo huo huo kutegemea misaada.
Kuna ishu ya maslahi duni na hii ndiyo imepelekea walimu wengi kujitumbukiza kwenye politiki. Huwezi amini mpaka mwaka 2000 nadhani maprofesa walikuwa wanalipwa around USD 1000. Motivation pale iko too low.
Ufisadi pia umechangia sana kupoteza muelekeo wa UDSM, Walimu, wafanyakazi wote ni kupiga dili tu kwa kwenda mbele.
All in all UDSM ina historia ya kujivunia na they can turn around in just few years kama kutakuwa na commitment ya kweli kutoka kwa owner, the state na pia appropriate leadership.