The future is here? Ijue "Starlink" na "Starlink Internet Satelite"

The future is here? Ijue "Starlink" na "Starlink Internet Satelite"

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747
Starlink ni hasa?

STARLINK ni mkusanyiko wa satellite za internet iliyobuniwa na kuwa chini ya mwanasayansi mashuhuli Elon Musk na timu yake ya SPACE X.

Mkusanyiko huo wa satellite za internet hufanya kazi kwa kushirikiana toka satellite moja had nyingine ili kutuma mawimbi ya mtandao huku duniani. Kampuni ya space x imedhamilia kutengeneza network ya mtandao wa satellite 12,000. Mpaka sasa starlink 650 tayari zipo kazini huku zaidi ya satellite 600 zikiwa zimeenelea kutumwa kwenye mzingo wa dunia toka mwezi may mwaka 2020, na nyingine 713 zikitegemewa kutumwa angani hivi karibuni.
images(2).jpg

Starlink iko umbali wa km550 toka ozone layer ya dunia. Kila satellite imeundwa ikiwa na antenna zenye nguvu kubwa inayoruhusu kutumwa na kupokea mawimbi ya mtandao kwa kasi kubwa kutokana na uwepo wa satellite hizo karibu zaidi na dunia. Internet ya satellite ni bora zaidi na kasi zaidi kuliko hii ya sasa inayotumika kwa sasa ya wire kwa sababu mawimbi ya satellite yatasafiri kwa 47% kasi kubwa sana kuliko inavyosafiri katika wire. Internet ya wire itaendelea kuwa haraka sana pindi inapotumika katika umbali mfupi.
images.jpg

Nia kuu ya internet ya starlink ni kutoa huduma za mtandao wa internet kwa maeneo yote duniani has yale ambayo hayajafikiwa na huduma za internet kabisa. STARLINK itatoa huduma ya internet kwa kasi ya karibia 300 Mbsp baadae mapema mwaka huu.

images(1).jpg
 
naona huko marekani ishaanza kufanya kazi
hulu bongo itafika link?
 
Back
Top Bottom